Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM aipa Wizara ya Fedha, Ujenzi siku 5
Habari za Siasa

JPM aipa Wizara ya Fedha, Ujenzi siku 5

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli ametoa siku tano kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango, kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa chelezo ya kujengea meli vilivyokwama bandari ya Dar es Salaam kwa sababu ya kodi, vinaachiliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo alipotembelea Bandari ya Mwanza, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chelezo, ukarabati wa meli 5 na ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria, unaogharimu zaidi ya Sh. 150 Bilioni, unaofanywa na kampuni 2 kutoka nchi ya Jamhuri ya Korea.

Rais Magufuli ameagiza wizara ya fedha iliyo chini ya Dk. Phillip Mpango na Wizara ya ujenzi iliyo chini ya Isack  Kamwelwe, kuhakikisha vifaa hivyo, ikiwemo na vifaa vya ukarabati wa meli, vilivyokwama kutokana na mchakato wa kikodi vinafikishwa katika Bandari ya Mwanza.

Aidha, Rais Magufuli amekasirishwa na ucheleweshwaji wa makontena 58 yenye vifaa vya ujenzi vilivyoagizwa na kampuni ya ukandarasi za Korea Total Marine Innovation (KTMI) na STK JV Saekyung Construction Ltd za Korea, kwa kusubiri msamaha wa kodi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagiza mitambo miwili ya kunyanyulia mizigo iliyokuwa imeuzwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kurejeshwa mara moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!