Jokate, Murro, Kafulila kumsaidia Rais Magufuli

RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, ambapo amemteua Mwanamitindo, Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe huku aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila akimteua kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Rais Magufuli amefanya uteuzi huo leo tarehe 28 Julai, 2018 na Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wengine walioteuliwa ni pamoja na Jerry Muro aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru wakati Patrobas Katambi akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.

Vile vile, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambapo Godfrey Chongolo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido akimteua kuirithi mikoba ya Hapi Kinondoni.

Na Lengay Ole Sabaya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Pia, Rais Magufuli amemteua Moses Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.

Hapa chini orodha kamili ya mabadiliko yaliyofanywa na Rais Magufuli

Katibu tawala

Abubakar Musa – Dar es Salaam
David Kafulila – Songwe
Denis Bandisa – Geita
Happy William – Iringa
Abdallah Malela – Katavi
Rashid Chatta – Kigoma

Masaile Mussa – Manyara
Carolin Mpapula – Mara
Dk. Jerry Mareko – Mtwara
Christopher Kadio – Mwanza
Eric Chitindi – Njombe
Riziki Salas – Ruvuma

Makatibu katika Wizara
Andrew Masawe – Ofisi ya Waziri Mkuu
Lisante Gabriel – Wizara Uvuvi na Mifugo
Dk. Jimmy James – Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi
Edwin Muhede – Wizara Viwanda Biashara na Uwekezaji

Wakuu wa Wilaya
Jerry Murro- Arumelu
Patrobas Katambi – Dodoma
Jokate Mwegero – Kisarawe

RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, ambapo amemteua Mwanamitindo, Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe huku aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila akimteua kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe. Anaripoti Regina Kelvin ... (endelea). Rais Magufuli amefanya uteuzi huo leo tarehe 28 Julai, 2018 na Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine walioteuliwa ni pamoja na Jerry Muro aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru wakati Patrobas Katambi akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma. Vile vile, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambapo Godfrey…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram