Jino kwa jino CCM vs Chadema

Spread the love

NI jino kwa jino, ndivyo unavyoweza kusema baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa pamoja kupiga yole la kuhujumiana. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Vyama hivyo vikuu vya ushindani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, vimekuwa vikitoleana tuhuma za kuchiana, kung’olea na hata kuandika maneno yasiyofaa juu ya mabango ya wagombea wao.

Taarifa kutoka katika vyama hivyo zimedai, mabango ya wagombea wao yamekuwa yaking’olewa usiku na kwamba, wanapoamka asubuhi hukuta yametoweka.

Wakati CCM ikituhumu wafuasi wa Chadema kung’oa na kusambaratisha mabango ya mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli mkoani Shinyanga, Iringa Chadema wanalia ‘kusafishwa’ kwa mabango yao.

Mabala Mlolwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga amelalamika kwamba, wafuasi wa Chadema wanang’oa mabango ya mgombea ursia wa chama hicho Dk. Magufuli.

“Sasa hivi kuna vijana wenu wameanza kuchana mabango ya mgombea wetu wa urais pia kuandika maneno machafu, hili siyo sawa kabisa. Naombeni vyama vya upinzani tufanyeni kampeni za kistaarabu ili uchaguzi uishe kwa amani,” amesema Mlolwa wakati wa uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Shinganya Mjini katika Kata ya Ngokolo.

Gasper Kileo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amedai, tayari wamefanya uchunguzi na matokeo ya awali yanaonesha kuwa, vijana hao wametoka Musoma na wamedhamiria kung’oa mabango yote ya chama hicho yaliyopo barabara kuu.

Huko Iringa, Brown Mwangomale, Katibu wa CCM wa mkoa huo amelalamikia wafuasi wa Chadema kwamba, wanameng’oa mabango ya wagombea wa chama hicho akiwemo mgombea urais wao, Dk. Magufuli.

“Tumeanza msako kwa ajili ya kubaini vijana waliohusika na kung’oa mabango ya wagombea wetu, tukiwakamata tutawafikishwa kwenye vyombo vya sheria,” amesema.

Mwangomale amesema, kila chama kinapaswa kuheshimu chama kingine na kuwa, kila chama kina haki ya kubandika mabango yake kokote hivyo ameeleza ustaarafu unapaswa kutawala katika kipindi hiki cha kampeni.

Mchungaji Peter Msigwa, mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, mbele ya Tundu Lissu ambaye ni mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, amedai wafuasi wa CCM wanang’oa mabango ya chama hicho.

“Wamekuwa wakienda kwenye maeneo yetu yalipo mabango ya wagombea wetu kisha wanayang’oa,” amesema na kuongeza “tunatahadharisha hili, hatuwezi kuvumilia vitendo hivi vya kihuni.”

NI jino kwa jino, ndivyo unavyoweza kusema baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa pamoja kupiga yole la kuhujumiana. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Vyama hivyo vikuu vya ushindani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, vimekuwa vikitoleana tuhuma za kuchiana, kung’olea na hata kuandika maneno yasiyofaa juu ya mabango ya wagombea wao. Taarifa kutoka katika vyama hivyo zimedai, mabango ya wagombea wao yamekuwa yaking’olewa usiku na kwamba, wanapoamka asubuhi hukuta yametoweka. Wakati CCM ikituhumu wafuasi wa Chadema kung’oa na kusambaratisha mabango ya mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli mkoani…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!