Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jiji la Arusha lawaonya wanaoleta vurugu
Habari za Siasa

Jiji la Arusha lawaonya wanaoleta vurugu

Spread the love

HALMASHAURI ya Jiji la Arusha, limeonya kuwachukulia hatua za kisheria wanaojihusisha na mgogoro wa maduka yake yaliyopo eneo la standi ndogo, anaandika Mwandishi Wetu.

Onyo hilo lilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Athuman Kihamia, kuwa baadhi ya watu wanachangia kuleta vurugu kati ya halmashauri, wamiliki wa maduka na wapangaji.

Amesema mgogoro huo ulishakwisha miezi miwili iliyopita na kufikia makubaliano kwa pande zote tatu ili kutafuta suluhu ambayo imesaidia kuepusha hali ya uvunjifu wa amani na watu kufanya biashara kwa mujibu wa sheria na makubaliano waliyojiwekea.

Amesema kuna baadhi ya wapangaji ambao wanachochea mgogoro huo kutokana kukataa kulipa malimbikizo ya kodi za nyuma wanazodaiwa hivyo wanadai kuwa maridhiano yaliyofanyika awali hawayatambui.

Onyo la Kihamia linafuatia viongozi wa wafanyabiashara kuzungumza na vyombo vya habari mwishoni mwa wiki iliyopitia wakimwomba Rais John Magufuli kusikiliza kilio chao na kuwasaidia kutatua mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.

Walidai muda wa miezi miwili hadi sasa maduka yao yamefungwa na watu wanaojiita wawekezaji wajenzi ambao wamewaamuru kuondoka.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara hao mwenyekiti wa wafanyabiashara wapangaji, Josephine Shirima, alisema mnamo Mei mwaka huu, watu waliojitambulisha kuwa ni wamiliki wa maduka hayo walifika majira ya usiku na kufunga maduka yao kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi hadi sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!