Edgar Lungu, Rais wa Zambia

Jeshi la Zambia lapambana na viwavi

ZAMBIA ipo katika sintofahamu baada la njaa inayotokana na uvamizi wa viwavi katika mashamba kwenye mikoa sita kati ya kumi inayounda nchi hiyo, anaandika Wolfram Mwalongo.

Hali hiyo imelilazimu Kikosi cha Jeshi la Anga kutumia ndege kunyunyiza dawa katika mikoa hiyo ili kunusuru mazao yaliyo mashambani.

Edgar Lungu Rais wa nchi hiyo amelitaka jeshi hilo kuhakikisha linatokomeza viwazi hivyo ambavyo kwa miaka minne iliyopita viliteketeza mazao na kusababisha taifa hilo kupata msukosuko baada ya kuishiwa na akiba ya chakula.

Mazao yaliyoathiriwa na viwavi hao ni mahindi, mihogo, mtama na mchele. Hata hivyo ndege za jeshi zimeanza kupuliza dawa hizo katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Zambia ina jumla ya watu milioni 16, imekuwa kwenye mdororo wa kiuchumi chini ya utawala wa Rais Lungu ambapo wachambuzi wa masuala ya uchumi wanadai hali ya uchumi wa taifa hilo kwa sasa inatofautiana na wakati taifa hilo likiongozwa na Rais Michael Sata aliyefariki dunia mwaka 2014.

Rais Sata wakati wa uhai wake alifanikiwa kuinua uchumi wa nchi yake pamoja na kupambana na ufisadi ingawa pia hakuweza kukwepa malalamiko kutoka kwa wapinzani wake.

ZAMBIA ipo katika sintofahamu baada la njaa inayotokana na uvamizi wa viwavi katika mashamba kwenye mikoa sita kati ya kumi inayounda nchi hiyo, anaandika Wolfram Mwalongo. Hali hiyo imelilazimu Kikosi cha Jeshi la Anga kutumia ndege kunyunyiza dawa katika mikoa hiyo ili kunusuru mazao yaliyo mashambani. Edgar Lungu Rais wa nchi hiyo amelitaka jeshi hilo kuhakikisha linatokomeza viwazi hivyo ambavyo kwa miaka minne iliyopita viliteketeza mazao na kusababisha taifa hilo kupata msukosuko baada ya kuishiwa na akiba ya chakula. Mazao yaliyoathiriwa na viwavi hao ni mahindi, mihogo, mtama na mchele. Hata hivyo ndege za jeshi zimeanza kupuliza dawa hizo katika maeneo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Masalu Erasto

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube