Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Jerry Murro: Alisema atajiua
Habari Mchanganyiko

Jerry Murro: Alisema atajiua

Spread the love

 

JERRY Murro, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha amesema, kijana Furahini Mbise, aliyekutwa amekufa katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Maweni, jijini humo aliwahi kusema “nitajiua.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Amesema, ameagiza Jeshi la Polisi pamoja na Daktari Kiongozi wa wilaya hiyo, kufanya uchunguzi ili kubaini nini kilitokea mpaka kijana huyo kupoteza maisha.

“Asili ya kijana huyu aliyekufa, hata ukiuliza kijijini, watakwambia kuina baadhi ya nyakati alisema anataka kujiua,” amesema Murro.

Akizungumzia mkasa ulivyokuwa, mkuu huyo wa wilaya amesema, Furahini alifariki dunia akiwa amehifadhiwa kwenye chumba kimoja kilichopo kwenye ofisi ya mtendaji huo kabla ya kujinyonga.

 “Taarifa zilizopo, kijana yule aliitwa saa 12 asubuhi kwa mwenyekiti wa kitongoji kuzungumza changamoto yao wenyewe ya mgogoro wa shami la kukatia majani.

“…na walipofika pale, kijana huyu ambaye amefariki, alileta vurugu. Alienda akachukua panga, mwenyekiti akaogopa akasema hili jambo liende kwa mtendaji,” amesema Murro.

Ameeleza, waliambiwa waende kwenye ofisi ya mtendaji kwa ajili ya kuzungumza jambo hilo.

“Taarifa zinaeleza, kijana yule alipofika ofisi ya mtendaji alileta vurugu, ndio wakaamua wamuweke kwenye chumba cha pembeni cha stoo, na alipowekwa kwenye chumba hicho habari zinasema, aliamua kujitundika, kujiua, kujinyonga,” amesema.

Kiongozi huyo amesema, awali alizungumza na ndugu wa marehemu akiwemo dada yake, pacha wa marehemu kama kulikuwa na mgogoro kati yake (marehemu) na mtendaji wa kata.

“Nikawauliza kama kulikuwa na mgogoro kati ya mtendaji wetu na marehemu, wakasema hapakuwa na mgogoro. Sasa iweje leo watu waseme amekwenda kwenye ofisi ya mtendaji, mtendaji akamuua? anaanzaje kumuua? mtu ambaye hakuwa na mgogoro naye?

“Lakini taarifa ambazo hazina mashaka, kijana huyu alikuwa na asili ya vurugu, ndio maana hata kwa mwenyekiti wa kitongoji jambo lake lilishindikana kusikilizwa, ndio likaletwa kwa mtendaji wa kata,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!