Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jenerali Mabeyo akosolewa
Habari za SiasaTangulizi

Jenerali Mabeyo akosolewa

Spread the love

MKUU wa jeshi la wananchi nchini (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo, amekoselewa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati, kufuatia kauli yake kuwa “jeshi la wananchi, litakabiliana” na anaowaita, “watoaji wa kauli za uchochezi ndani ya nchi.” Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE kwa njia ya simu, leo tarehe 13 Aprili, mbunge wa Bukoba Mjini, Willifred Lwatakare amesema, kauli ya Jenerali Mabeyo, imelenga kutaka jeshi kujiingiza katika masuala ya kisiasa.

Anasema, “bila shaka, kwamba Jenerali Mabeyo, anataka kuliingiza jeshi la wananchi kwenye ulingo wa kisiasa, ili kunufaisha Chama Cha Mapinduzi (CCM).”

Anaongeza, “kauli yake, kwamba ‘majeshi yamejipanga kukabiliana na vitendo na kauli za uchochezi, zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa,’ ni ushahidi wa hiki ninachokieleza.”

Jenerali Mabeyo na hata Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanajua kuwa hakuna namna ambayo chama hicho kinaweza  kushinda katika uchaguzi ujao, bila kutumia vitisho kutoka kwa majeshi yetu. 

Aidha, katika baadhi ya mitandao ya kijamii, watu mbalimbali wamekosoa kauli ya Jenerali Mabeyo, kutaka kulitumia jeshi kukabiliana na wanasiasa.

Akihutubia wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa mji wa kiserikali, uliyopo Chamwino, mjini Dodoma, Jenerali Mabeyo, amenukuliwa akisema, “jeshi limejipanga kukabiliana na vitendo vya uchochezi vinavyohatarisha usalama wa nchi.”

Huku akishangiliwa na wanaohisiwa kuwa wanachama wa chama kimoja cha siasa nchini, Jenerali Mabeyo alisema, “tunaendelea kufuatila kauli tata zenye kuashiria ishara za uchochezi. Tuko tayari kukabiliana na vitendo vyovyote vitakavyotokana na uchochezi huo ndani ya nchi yetu.”

Akizungumzia migogoro inayoendelea katika baadhi ya nchi jirani, Jenereali Mabeyo, ameeleza kuwa jeshi liko tayari kuilinda nchi, iwapo migogoro hiyo itaonekana kuiathiri kwa namna yoyote ile Tanzania.

Alisema, “migogoro inayofukuta katika nchi jirani inaweza ika (influence) kuleta hali isiyotabirika katika nchi yetu. Nikuhakikishie mheshimiwa Rais (Rais John Magufuli), tuko tayari kuilinda nchi yetu.

“Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, tuko tayari kulinda wananchi na mali zao; na tuko mstari wa mbele kushirikiana na wenzetu.”

Jenerali Mabeyo hakuzitaja nchi jirani ambazo zimekumbwa na migogoro ya kisiasa.

Hata hivyo, juzi Alhamisi, jeshi nchini Sudan ya Kaskazini –   Khartoum – lilitangaza kumaliza miongo mitatu ya utawala wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Omar al-Bashir.

Rais al-Bashir alilazimishwa na jeshi la Sudan kuondoka madarakani, kufuatia maelfu ya wananchi wake, kufanya maandamano ya kupinga utawala wake.

Maandamano ya wananchi wa Sudan, kupinga utawala wa al- Bashir, yalianza Desemba mwaka jana. Hadi sasa, pamoja na rais al-Bashir kung’olewa mamlakani, bado wananchi wanaendelea kuandamana. Safari hii, wanapinga hatua ya jeshi kutwaa madaraka.

Kiongozi huyo wa muda mrefu alipinduliwa na kukamatwa siku ya Alhamisi, baada ya miezi kadhaa ya maandamano.

NayeTito Magoti, Mtafiti na Mwanaharati wa Haki za Binadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ameandika yafuatayo katika ukurasa wake wa twitter, kupinga kauli ya Jenerali Maboye.

Amesema: “General hii sio kazi ya jeshi letu tunaloliheshimu sana. JWTZ na uchochezi wapi na wapi? Kwa hiyo, JWTZ imeanzisha kitengo cha upelelezi na uendesha mashitaka? Askari wa JWTZ wataenda mahakamani? Tumikeni kwa kiasi. Watanzania sio wajinga kiasi hicho.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!