January 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Japan, Australia kusaini ushirikiano wa ulinzi dhidi ya China

Ndege ya kivita ya India

Spread the love

KATIKA juhudi za kudhibiti kukua kwa ushawishi wa China katika Pwani ya Kusini mwa nchi hiyo, Waziri Mkuu wa Japan, Yoshihidi Suga na mshirika wake Scott Morrison wa Australia wanatarajiwa kutiliana saini makubaliano katika ulinzi hivi karini, taarifa zinaeleza. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Morisson aliwasili Japan, Jumanne iliyopita ambapo wataalamu wa masuala ya Ulinzi na Usalama, wanamtarajia kuhitimisha mkataba wa ushirikiano katika Mafunzo na Shughuli za Kijeshi (RAA) na Mshirika wake Suga.

Lengo la mkataba huo ni kuweka mfumo wa kisheria wa vikosi vya kijeshi, kutoka pande mbili hizo kutembeleana ili kutengeneza ushirika katika mafunzo na operesheni za kijeshi.

“Kutakua na jambo la kuwaeleza kutoka katika mkutano wetu,” alisema Ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Japan katika mkutano na waandishi wa habari na kuongeza;

“Mazungumzo ya mkataba huu wa ulinzi, yamechukua miaka sita na yanahitaji kuthibitishwa na wanasheria wa pande zote mbili.”

 

Aidha, wataalam wa ulinzi na usalama wanaamini kwamba, Japan na Australia zinatafuta mfungamano wa karibu wa kijeshi kutokana na kukua kwa hofu juu ya kuongezeka kwa operesheni za kijeshi za China katika ukanda huo wa Pwani ya Kusini ya nchi hiyo.

Shughuli hizo za kijeshi za China ni pamoja na kuweka wanajeshi katika Pwani ya Kusini ya China, kuingia kiujanja karibu na visiwa vyenye mgogoro vya Pwani ya Mashariki ya China  na China kuongeza duru zake katika mataifa ya visiwa vya Pasifiki vya Mashariki ya Mbali.

Joe Biden, Rais Mteule wa Marekani

“Makubaliano haya yatasaidia mataifa mengine kuwajibika zaidi katika shughuli na oparesheni za kijeshi katika ukanda huu, sio kwa uchache kama wamarekani wanavyonyooshwa,” alisema Grant Newsham, Mtafiti katika Baraza la Mafunzo ya Kimkakati la Japan.

Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Toshimtsu Motegi alisema Jumatatu iliyopita kuwa, nchi yake itamuomba rais mpya wa Marekani, Joe Biden kuweka mkazo katika sera za nje ikiwa ni pamoja na kuweka utulivu katika ukanda huo.

“Japan ina changamoto kubwa katika kuhakikisha kuwa Marekani inaendelea kujitolea kuweka utulivu katika ukanda wa Pasifiki, kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi, ulinzi na usalama na mambo mengine ya kidunia,” Motegi aliwaambia wanahabari katika ofisi za Chama cha Waandishi wa habari Japan.

Alisema, Japan lazima iendelee kufanya juhudi ili  kuidhibiti China  kutokana na kukithiri ongezeko la vikosi vyake vya majini katika Pwani ya Kusini na Mashariki ya China.

“Japan inahitaji kujilinda na majaribio ya China ya kutaka kubadilisha heshima yake katika Pwani ya Kusini na Mashariki ya China kwa nguvu”, alisema Motegi.

error: Content is protected !!