Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam

Janga la Corona:Tanzania yazuia safari za ndege kimataifa

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA), imefuta safari za ndege za abiria za kimataifa, huku ikiweziwekea masharti ndege za mizigo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Zuio hilo limetolewa na TCAA jana tarehe 11 Aprili 2020, huku ikieleza sababu zake kuwa ni kudhibiti kasi ya ueneneaji Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19).

Kwa mujibu wa taarifa ya TCAA, zuio hilo litadumu hadi mamlaka hiyo itakapotoa taarifa zaidi.

“Kutokana na janga la COVID-19, vikwazo vifuatavyo vimechukuliwa kuanzia Aprili 11 2020 hadi taarifa zaidi itakapotolewa. Ratiba zote za safari za kimataifa zimesitishwa,” inaeleza taarifa ya TCAA.

TCAA imeeleza kuwa, ndege za mizigo zitaruhusiwa kufanya safari, lakini zitapaswa kuwa na watu wachache ambao watawekwa karantini na serikali,  kwa gharama zao.

SERIKALI ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA), imefuta safari za ndege za abiria za kimataifa, huku ikiweziwekea masharti ndege za mizigo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam ... (endelea). Zuio hilo limetolewa na TCAA jana tarehe 11 Aprili 2020, huku ikieleza sababu zake kuwa ni kudhibiti kasi ya ueneneaji Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Kwa mujibu wa taarifa ya TCAA, zuio hilo litadumu hadi mamlaka hiyo itakapotoa taarifa zaidi. "Kutokana na janga la COVID-19, vikwazo vifuatavyo vimechukuliwa kuanzia Aprili 11 2020 hadi taarifa zaidi itakapotolewa. Ratiba zote za safari za…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!