Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Janga la Corona: NIMR yatafiti chanzo vifo wenye magonjwa sugu
AfyaHabari Mchanganyiko

Janga la Corona: NIMR yatafiti chanzo vifo wenye magonjwa sugu

Prof. Yunus Mgaya, Mkurugenzi Mkuu NIMR
Spread the love

TAASISI ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini (NIMR) nchini Tanzania, inafanya utafiti kubaini chanzo cha watu wenye magonjwa sugu, kuathirika zaidi na ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi tarehe 9 Mei 2020 jijini Dar es Salaam na Profesa Yunus Mgaya, Mkurugenzi Mkuu NIMR, wakati akizungumza na wanahabari.

Prof. Mgaya ameyataja magonjwa hayo kuwa ni, kisukari, shikizo la damu, Virusi vya Ukimwi (VVU), saratani na ugonjwa wa moyo.

Mwanzoni mwa mwezi Aprili 2020, Dk. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri wa Afya, aliwataja wenye magonjwa hayo, kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kutokana ugonjwa huo na Covid-19, na kuwataka wazingatie ushauri unaotoka kwa watalaamu wa afya.

Kufuatia tahadhari hiyo, Prof. Makubi amesema katika utafiti wa NIMR,  taasisi hiyo inatafiti matatizo yanayopelekea wenye magonjwa hayo kuathirika zaidi, ikiwemo baadhi yao kupoteza maisha.

“Tunangalia wenye magonjwa hayo kama wakiwa na maambukizi wanakuwa na matatizo  gani, kwa hiyo tuna utafiti ambao unaendelea,  unaoangalia wagonjwa hao  ili kuona wanaathirika kiasi gani kwa corona,” amesema Prof. Mgaya.

Prof. Mgaya amefafanua kuwa, wagonjwa hao wakipata maambukizi ya Covid-19 wanashindwa kupambana nao kutokana na kinga zao za mwili kuwa ndogo. Hivyo wanaofariki dunia, hawapotezi maisha kwa sababu ya Corona, bali kutokana na maradhi yao yaliyokuwepo awali.

“Tunafahamishwa kwamba kuna wananchi wana magonjwa yasiyo ya kuambukizwa, kinga zao za mwili zinashuka,  kwa hiyo wakipata corona wanafariki kwa hayo magonjwa na si corona,” amesema  Prof. Mgaya.

Wakati huo huo, Prof. Mgaya amesema NIMR inafanya tafiti takribani tisa kuhusu ugonjwa huo, ikiwemo utafiti kubaini mwenendo wa maambukizi ya Covid-19, na namna wananchi wanavyotekeleza ushauri wa kitaalamu juu ya kujikinga nao.

“Kama taasisi tumejikita katika tafiti tisa tayari, ambazo ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji, na lengo kubwa kupata majibu katika masuala mbalimbali ambayo sisi tunajiuliza na wanaohudumia wagonjwa wanashuhudia na haya majibu tutayapata baada ya utafiti,” amesema Prof. Mgaya.

Prof. Mgaya amesema taasisi hiyo itakapokamilisha tafiti hizo, itatoa matokeo yake kwa umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!