UPANDE wa Mashtaka katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando kuanza kumuuliza maswali mtuhumiwa huyo ifikao Oktoba 16 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Tarehe hiyo, upande wa Jamhuri utaanza kumuuliza maswali Tido dhidi ya utetezi wake alioutoa tarehe 20 Septemba 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kabla ya tarehe hiyo kupangwa, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi aliiahirisha kesi hiyo ambayo ilitakiwa kuendelea leo, kufuatia Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai kupata udhuru.
Tido anayetuhumiwa kuisababishia serikali hasara ya Sh. 887.1 milioni kutokana na matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa mkurugenzi wa TBC, alitakiwa kuulizwa maswali na upande wa jamhuri baada ya upande huo kufunga ushahidi baada ya mashahidi wake akiwemo Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa, Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa TBC, Clement Mshana pamoja na Ofisa Uchunguzi wa TAKUKURU kutoa ushahidi wao kwenye kesi hiyo.
Leave a comment