Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba

Jaji Warioba: Muwapishe wengine madarakani

JAJI Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu amewashauri viongozi wa umma kutokaa madarakani muda mrefu, akisema kwamba kitendo hicho hakina tija kwa masilahi ya taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Jaji Warioba ametoa ushauri huo leo tarehe 14 Oktoba 2019, wakati akizungumza katika Kongamano la Kumbukizi ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Jaji Warioba ameeleza kuwa, kitendo cha baadhi ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, kinasababisha ufanyaji kazi kwa mazoea, na kuathiri maendeleo ya nchi.

Na kushauri viongozi walioko madarakani muda mrefu, kuwapisha wengine.

“Usikae madarakani muda mrefu utakua na uzito wa kufanya kazi kwa wakati, utaanza kufanya kazi kwa mazoea. Kufanya kazi kwa mazoea haileti maendeleo, inatakiwa ifike mahali, unawapisha wnegine,” amesema Jaji Warioba.

Akizungumzia miaka 20 ya Tanzania bila ya Mwalimu Nyerere, Jaji Warioba amesema alikuwa anafuata sheria na kupenda ushauri kutoka kwa wengine.

“Nyerere alikuwa anapenda kufuata sheria, alikuwa mtu wa kawaida, wa kushaurika,” amesema Jaji Warioba.

JAJI Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu amewashauri viongozi wa umma kutokaa madarakani muda mrefu, akisema kwamba kitendo hicho hakina tija kwa masilahi ya taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Jaji Warioba ametoa ushauri huo leo tarehe 14 Oktoba 2019, wakati akizungumza katika Kongamano la Kumbukizi ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika Wilaya ya Butiama mkoani Mara. Jaji Warioba ameeleza kuwa, kitendo cha baadhi ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, kinasababisha ufanyaji kazi kwa mazoea, na kuathiri maendeleo ya nchi. Na kushauri viongozi walioko madarakani muda mrefu, kuwapisha wengine. “Usikae madarakani muda mrefu utakua na uzito wa kufanya kazi…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram