Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jaji Mutungi aionya Chadema kunajisi katiba, sheria
Habari za Siasa

Jaji Mutungi aionya Chadema kunajisi katiba, sheria

Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania
Spread the love

JAJI Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, amekionya Chama Kikuu cha Upinzani nchini huko Chadema kuacha kukiuka Katiba na Sheria za nchi hiyo kuwa kunanajisi Wimbo wa Taifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Jaji Mutungi ametoa onyo hilo leo Jumanne tarehe 4 Oktoba 2020, wakati anazungumza na wanaandishi jijini Dar es Salaam.

Mlezi huyo wa vyama vya siasa amedai, Chadema kimefanya uvunjifu huo kwa makusudi, ilihali kikijua kwamba ni kinyume na Katiba na Sheria za nchi.

“Kilichonisikitisha, kitendo cha kufanya uvunjifu wa sheria kwa makusudi. Kilichofanyika na Chadema kuchukua Wimbo wa Taifa na kuongeza aya ya tatu na mbaya zaidi wanasema tunaongeza tuone yanayotokea, sikutegemea chama cha siasa kikongwe kifanye uvunjifu ule halafu tukae kimya,” amesema Jaji Mitungi.

Licha ya kutoa onyo hilo, Jaji Mutungi amesema, Wizara ya Mambo ya Ndani inafuatilia kwa ukaribu suala hilo.

“Kwa hili lilofanyika ni kama kunajisi Wimbo wa Taifa. Naamini kuna taasisi inahusika iko ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani, naamini hawawezi kukurupuka kuchukua hatua wanafuatilia jambo hili,” amesema Jaji Mutungi.

Aidha, Jaji Mutungi, ameitaka Chadema kufanya mkutano wake mkuu leo Jumanne kwa amani na kuepuka vitendo vitakavyovunja sheria za nchi.

Mkutano huo unafanyikia ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Nawaonya Chadema wakati wanaendelea na mkutano wao wahehsimu sheria za nchi,” amesema Jaji Mutungi.

“Kama tunataka kuenzi amani. Tume inajitahidi kushirikisha wadau katika maandalizi ya uchaguzi kuhakikisha tunaingia uchaguzi kwa amani kutokana na kauli ya Rais John Magufuli kwamba uchagui huu utakua huru, haki na amani.”

“Tunapovunja sheria bado nasikitika hasa kiongozi wa chama anasema, tunaongeza aya ya tatu tuone kinachotokea kwa akili ya kawaida sidhani kama kiongozi mwenye maono ya kuienzi amani ya nchi anaweza kusema hivyo,” amesema Jaji Mutungi.

Jaji Mutungi ameviataka vyama na wadau wa siasa kufuata sheria za nchi ili kuepusha vitendo vya uvunjifu wa amani hasa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

“Nichukue azma hii kuvisihi vyama vijaribu kuheshimu sheria za nchi, vinginevyo sheria itachukua mkondo wake. Naamini anayevunja sheria, sheria itachukua mkondo wake juu yake,” ameonya Jaji Mutungi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!