Jaji Mkuu Rasmi Kuanza Kazi – MwanaHALISI Online
Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Hamis Juma akila kiapo
Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Hamis Juma akila kiapo

Jaji Mkuu Rasmi Kuanza Kazi

Rais wa Tanzania  Dkt John Mgufuli, amemwapisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Hamis Juma, ambapo awali alikuwa akikaimu nafasi alikuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, baada ya aliyekuwa Jaji Mkuu kustaafu kisheria, Mohamed Othman Chande, anaandika Irene david.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika shughuli za kuapishwa zilizofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Jaji Ibrahim amesema ataendeleza misingi mizuri waliyoiacha majaji wakuu waliopita ikiwemo kupambana na rushwa katika taifa na pia kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa mahakama katika mikoa mbalimbali nchini.

Aidha ameongezea kwa kusema kuwa atasimamia haki kama sheria inavyoitaka Mahakama kutoa haki kwa raia wote nchini.

“Tatizo la uhaba wa mahakama ya mwanzo nchini imekuwa ni changamoto na kwamba tayari mikakati ilishawekwa na Jaji aliyepita hivyo kilichobaki ni utekelezaji na kuwa utafanikiwa mpango huo,” amesema Jaji Ibrahim.

Rais wa Tanzania  Dkt John Mgufuli, amemwapisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Hamis Juma, ambapo awali alikuwa akikaimu nafasi alikuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, baada ya aliyekuwa Jaji Mkuu kustaafu kisheria, Mohamed Othman Chande, anaandika Irene david. Akizungumza leo na waandishi wa habari katika shughuli za kuapishwa zilizofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Jaji Ibrahim amesema ataendeleza misingi mizuri waliyoiacha majaji wakuu waliopita ikiwemo kupambana na rushwa katika taifa na pia kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa mahakama katika mikoa mbalimbali nchini. Aidha ameongezea kwa kusema kuwa atasimamia haki kama sheria inavyoitaka Mahakama kutoa haki kwa raia wote…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Irene David

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube