RAIS wa Iran, Hassan Rouhani ameahidi kupinga vikwazo vya Marekani dhidi ya taifa lake, vinavyotarajiwa kuanza kutekelezwa leo tarehe 5 Novemba 2018. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Mwishoni mwa wiki iliyopita Marekani ilitangaza kuibua vikwazo vya zamani na kuanzisha vikwazo vipya dhidi ya Iran, huku vikwazo hivyo vikilenga sekta ya taasisi za kifedha, mafuta, gesi, usafirishaji wa majini.
Akihutubia baraza la mawaziri la Iran leo Jumatatu, Rais Rouhani amesema Iran imetengeza sera za kufuta vikwazo vya Marekani.
Amelitaka baraza hilo kuhakikisha kwamba Marekani inaelewa kwa lugha rahisi kwamba, hawawezi kushughulika na taifa lao kwa kutumia nguvu, shinikizo na vikwazo.
Rouhani amejigamba kuwa, kitendo cha Marekani kuziondoa nchi nane zinazonunua mafuta ya Iran katika vikwazo vyake, ni ushindi kwa taifa lake.
“Jamhuri ya Kiislam ya Iran inaweza kuuza mafuta yake hata kama nchi nane hazijaondolewa kwenye vikwazo,” amesema Rouhani.
Leave a comment