India wapiga marufuku kuacha mke – MwanaHALISI Online
Pre-Matrimonial-Investigation-Large

India wapiga marufuku kuacha mke

SERIKALI ya India imeanza utekelezaji wa muswada wa sheria ya ulinzi wa haki katika Ndoa wa mwaka 2017 uliokwama kupitishwa na bunge la nchi hiyo, ambao unalenga kuwabana wanaume wa kiislamu kutoa talaka tatu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Muswada huo ambao unatafisri utolewaji wa talaka tatu za papo kwa papo kama kosa la jinai ambapo mhusika anaweza kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, ulikwama kupitishwa bungeni mwezi Agosti 2018 baada ya pande zote mbili (upinzani na serikali) kukosa makubaliano.

Muswada huo uliowasilishwa bungeni na serikali ya Narendra Modi ulikwama kupitishwa kutokana na kutopigiwa kura na wabunge wengi.

Akizungumza na wanahabari jana Waziri wa Sheria India, Ravi Shankar Prasad alisema serikali ya nchi hiyo imeamua kuanza utekelezaji wa sheria hiyo baada ya kukithiri kwa matukio ya utolewaji wa talaka hizo licha ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama kuu ya nchi hiyo kuhusu usitishaji wa talaka hizo kutokana na kuwa kinyume na katiba ya India.

Hata hivyo, Vyama vya Upinzani India vimekosoa vikali uamuzi huo vikidai kuwa, baadhi ya masharti yaliyomo katika muswada huo ni magumu kutekelezeka.

SERIKALI ya India imeanza utekelezaji wa muswada wa sheria ya ulinzi wa haki katika Ndoa wa mwaka 2017 uliokwama kupitishwa na bunge la nchi hiyo, ambao unalenga kuwabana wanaume wa kiislamu kutoa talaka tatu. Anaripoti Regina Kelvin ... (endelea). Muswada huo ambao unatafisri utolewaji wa talaka tatu za papo kwa papo kama kosa la jinai ambapo mhusika anaweza kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, ulikwama kupitishwa bungeni mwezi Agosti 2018 baada ya pande zote mbili (upinzani na serikali) kukosa makubaliano. Muswada huo uliowasilishwa bungeni na serikali ya Narendra Modi ulikwama kupitishwa kutokana na kutopigiwa kura na wabunge wengi. Akizungumza na…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Regina Mkonde

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube