Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Imevuja; CAG ‘aliilewesha’ kamati iliyomuhoji
Habari za SiasaTangulizi

Imevuja; CAG ‘aliilewesha’ kamati iliyomuhoji

Prof. Mussa Assad, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali
Spread the love

TAARIFA kutoka ndani ya kamati iliyomuhoji Prof. Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) jana Jumatatu, ‘ilibaki mdomo wazi’. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maadili amesema kuwa, Prof. Assad ni mtu makini ‘mno’ na kwamba alikuwa na majibu yaliyonyooka kwa kila swali jambo lililotosheleza wajumbe.

“Huyu anajua alichokifanya na ndio maana aliweza kujibu vizuri kila swali aliloulizwa jambo lililomtosheleza kila mmoja wetu, kila mmoja wetu alikuwa kiu yake,” ameeleza na kuongeza;

“Hatukutarajia kama atakua muungwana kwa kiwango alichoonesha. Hakuwa na hasira hata kidogo na alibaini maswali ya mtego ambayo aliyajibu vizuri.”

Pamoja na chanzo hicho kueleza kwa uchache mazingira ya kikao hicho, hakua tayari kueleza mjadala wenyewe na mwisho wake.

“Naweza kukwambia nini kimejiri lakini sitofanya hivyo kwa kuwa taarifa inapaswa kutoka kwa Spika baada ya kukabidhi ripoti hii,” kimeeleza chanzo hicho.

Yaliyoelezwa na chanzo hiki yanapata nguvu kutokana na kauli ya makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Dk. Christine Ishengoma.

“Shahidi wetu ametoa ushahidi mkubwa sana. Tumemuhoji na amerujibu maswali yetu kama alivyoulizwa,” alisema Dk. Ishengoma baada ya kumaliza mahojiano na CAG.

Hata hivyo chanzo hichi kimeeleza kuwa, katika mahojiano hayo kilichotawala ni uungwana kwa pande zote mbili yaani upande wa shahidi na kamati.

“Tofauti kabisa na taarifa za awali katika vyombo vya habari na mitandaoni, hakuna jambo lililoinekana kuwa gumu kwenye kikao hicho.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!