March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ihefu kuanza na Simba Ligi Kuu, Yanga na Tanzania Prisons

Spread the love

BODI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) 2020/21, imetangaza ratiba ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 18. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pazia la ligi hiyo litafunguliwa tarehe 6 Septemba, 2020 kwa michezo sita kupigwa katika viwanja tofauti, huku mechi tatu zitapigwa tarehe 7.

Mabingwa wa watetezi wa ligi hiyo, Simba wao wataanzia ugenini kuumana na wageni wa VPL, timu ya Ihefu inayotumia dimba la Sokoine jijini Mbeya kama uwanja wake wa nyumbani.

Timu ya Yanga yenyewe itaanzia nyumbani, ikiikaribisha timu ya Tanzania Prison, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!