Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Idris asota siku 5 rumande, Polisi warushiana mipira
Habari MchanganyikoMichezo

Idris asota siku 5 rumande, Polisi warushiana mipira

Spread the love

IDRIS Sultani, Msanii wa vichekesho nchini Tanzania, anaendelea kusota rumande, katika Kituo cha Polisi  cha Oysterbay jijini Dar es Salaam, kwa kosa la kuidhihaki picha ya Rais wa nchi hiyo, John Pombe Magufuli. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Leo Jumamosi tarehe 23, Mei 2020, Idris anafikisha siku tano akisota rumande, tangu aliposhikiliwa tarehe 19 Mei 2020, baada ya kujisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, kufuatia kusambaa kwa video inayomuonesha akiicheka picha ya Rais Magufuli, mitandaoni.

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE kwa simu leo, Benedict Ishabakaki, Wakili wa Idris, amesema, polisi waliahidi kumpa dhamana jana Ijumaa msanii huyo, lakini baadae walikataa bila ya kutoa sababu.

Wakili Ishabakaki amesema, anaendelea kufuatilia dhamana ya msanii huyo.

“Jana, walikataa kutoa dhamana na hawajatoa sababu. Wakishakwambia hakuna dhamana ina maana kesho yake unafuatilia tena, hivyo leo nafuatilia dhamana maana wanatoa siku yoyote,” amesema Wakili Ishabakaki.

Wakili Ishabakaki amesema, baada ya Idris kunyimwa dhamana, alirudishwa katika Kituo cha Oysterbay, baada ya kuhojiwa ofisi ndogo za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.

MwanaHALISI OLINE limezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu kwa simu kuhusu dhamana ya msanii huyo, amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa linachunguzwa na makao makuu ya jeshi hilo.

Idriss Sultan

“Niko maeneo ya mbali, lakini hilo shauri siwezi kuzungumzia sababu linachunguzwa na makao makuu ya polisi na niko mbali na maeneo ya tukio sina uhakika.”

“Siwezi kuwa na mawasiliano ya haraka haraka kwa sasa hivi na sina uhakika kama bado yuko Oysterbay au la ameachiwa,” amesema Kamanda Taibu.

MwanaHALISI ONLINE limemtafuta, David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania kuhusu kinachoendelea juu ya Idris ikiwamo dhamana,  amesema anafuatilia suala hilo.

“Ngoja nifuatilie, kisha nitakupigia simu,” amesema SACP Misime.

Kwa mujibu wa wakili wa Idris, alisema mteja wake anakabiliwa na kosa la uonevu kwa njia ya mtandao, ambapo anatuhumiwa kuicheka picha ya zamani ya Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!