Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ibada kuaga mwili wa Mkapa Dar, Rais Magufuli ashiriki
Habari za SiasaTangulizi

Ibada kuaga mwili wa Mkapa Dar, Rais Magufuli ashiriki

Misa ya kumuaga mwili wa Rais Benjamin Mkapa
Spread the love

MAMIA ya wananchi wamejitokeza kwa wingi Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kuuaga mwili wa Hayati Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mwili wa Mkapa aliyefariki dunia Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 umewasilia uwanja hapo saa 4 asubuhi ukitoka Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.

Leo Jumapili tarehe 26 Julai 2020, kunafanyika shughuli ya kuuaga mwili huo ikitanguliwa na misa maalum ambayo imekwisha kuanza ikihudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Pia, Anna, mjane wa Mkapa, ndugu, jamaa na marafiki wamejitokeza kuhudhuria misa hiyo.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Thaddeus Ruwa’ichi ametoa nia ya misa hiyo maalum kwa ajili ya kumwombea Hayati Mkapa.

Ibada hiyo inaongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Mhasham Tarcisius Ngalalekumtwa.

Pia, imehudhuriwa na maaskofu wengine; Agapiti Ndorobo wa Jimbo la Mahenge na Anthony Banzi wa Jimbo la Tanga.

Shughuli ya kuaga mwili huo, itafanyika kwa siku tatu leo hadi Jumanne tarehe 28 Julai 2020 kisha mwili huo utasafirishwa kwenda kijijini kwake, Lupaso, Masasi Mkoa wa Mtwara kwa maziko yatakayofanyika Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Viongozi wengine waliopo ni; Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Miwnyi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!