Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Huu ndiyo mpango mkakati wa miaka mitano ya EWURA
Makala & Uchambuzi

Huu ndiyo mpango mkakati wa miaka mitano ya EWURA

Titus Kaguo, Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano (EWURA)
Spread the love

ILI UWEZE kufanikisha jambo ni lazima uweke mipango mikakati ya jambo ambalo unataka kulifanya kwa maana ya mpango wa mrefu wa kati na wa muda mfupi. Anaandika Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Na mipango hiyo ufanywa katika mamlaka mbalimbali zenye nia ya kuboresha huduma zake, serikali, familia au mtu binafsi ambaye anakitambua na kutambua anachotaka kukifanya.

Hali hiyo imeweza kubainishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)  ambayo ni moja ya Mamlaka za Udhibiti nchini ambayo ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ya mwaka 2001 (Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania) pamoja na majukumu mengine, kupewa majukumu chini ya Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 (Sura ya 392 ya Sheria za Tanzania) kudhibiti shughuli za mkondo wa kati na wa chini wa petroli (yaani mafuta na gesi asilia) katika Tanzania Bara.

Kutokana na maelezo hayo sasa kila msomaji ataweza kuelewa EWURA ni nini na inafanya kazi gani kwa mazingira gani na kwa mipaka gani na kwa maana hiyo sasa tuangalie mikakati ya EWURA kwa kipindi cha miaka mitano (2018/19 -2021/22)

Mpango Mkakati wa miaka mitano ulioanza 2018/19 mpaka Juni 2023 ulitengenezwa kupitia michakato ya maingiliano na ushirikishi, Kupitia mfululizo wa semina za mipango ya maingiliano ya kimkakati, kazi za EWURA na shughuli zake zilitengenezwa ili kuleta mambo muhimu ambayo yanaathiri utoaji wa huduma za EWURA, ubora na udhaifu wake.

Mchakato huu wa maingiliano ulilenga kutengeneza uelewa wa pamoja juu ya mchakato wa kuandaa mpango mkakati na matokeo yake ya baadaye.

EWURA ilianzisha warsha za kuunda mpango mkakati huu zilijumuisha uchambuzi wa mambo mbalimbali kama vile  Chimbuko la EWURA, Kazi na majukumu ya EWURA.

Kutokana na hali hiyo ilifanyika  Tathmini ya matokeo ya Mpango Mkakati uliopita ikiwa ni pamoja na kufanya uchambuzi wa mipango ya hivi karibuni, mafanikio na changamoto zake na mambo yaliyofanyiwa tathimini na uchambuzi ni pamoja na

Uchambuzi wa wadau, Mapitio ya Shirika na Tathimini ya uelekeo wa taasisi

Hata hivyo uchambuzi huo ulitokana na mambo muhimu ambayo ni kufikiria kuwa katika kipindi cha kupanga mkakati huu, EWURA itahitaji kukutana na changamoto mpya kila wakati na maagizo ya serikali, hivyo EWURA itajipambanua kila wakati ili kukabiliana na changamoto hizo.

 Muingiliano wa kijinsia (Gender Mainstreaming), utawala bora, VVU / UKIMWI, magonjwa yasiyoambukiza, afya na utimamu wa wafanyakazi, unywaji wa dawa za kulevya na pombe na ulinzi wa mazingira, vitaendelea kushughulikiwa na kuimarishwa katika Mpango Mkakati huu.

Pia ilionekana kuwa ili EWURA iweze kufikia matarajio ya wadau, Mamlaka itahitaji kupitisha mikakati itakayoongeza uwezo wa Mamlaka wa kupata, kuchambua na kusambaza taarifa kwa ajili ya kufanya maamuzi.

Kwa kuongezea, EWURA itahitaji kuunda mfumo wa kupata habari kutoka kwa sekta za usimamizi ili kusimamia vyema na wakati huo huo, kuwa na huduma zenye uwazi na kuweka viwango vya huduma vinavyotarajiwa na wadau wake (mkataba wa huduma kwa Wateja na kupata mrejesho),

 Serikali kuendelea kuchukua hatua za kuboresha mazingira ya biashara nchini Tanzania. Ili kutekeleza juhudi hiyo na  EWURA itaendelea kukuza zana za kisheria zilizopo kwa ajili ya kuvutia uwekezaji katika sekta husika.

Jambo lingine ilionekana ili kuweza kushughulikia uwekezaji duni katika sekta husika, EWURA itaongeza juhudi zake za kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi na Ushirikiano wa Umma na Sekta Binafsi (PPPs),

Aidha ilifikiriwa masuala ya mtaji wa rasilimali watu ikiwa ni pamoja na ukuzaji wa wafanyakazi, ushiriki wao, kuzingatia utamaduni wa taasisi, kuajiri, kuboresha mazingira ya kufanya kazi, vitaendelea kuwa muhimu ili kuhakikisha kuwa, EWURA inakuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa kasi na ubora unaokubalika,

Katika uchambuzi huo ilionekana ufadhili wa kifedha kwa EWURA ni eneo lingine la kipaumbele kwenye Mpango Mkakati huu, kwa sababu shughuli za EWURA zinapopanuka, ufadhili wa kifedha utakuwa muhimu zaidi. Ni muhimu kwa EWURA kuwa na nguvu za ifedha kama ilivyoainishwa katika Sheria ya EWURA, Sura ya 414.

Jambo lingine la uhimu ni Umma lazima ujue na kushiriki katika mchakato wa kusimamia sekta za nishati na maji, Elimu kwa Umma na uhamasishaji utaendelea  vitaendelea kushughulikiwa katika Mpango Mkakati huu.

Elimu kwa umma na uhamasishaji

EWURA imepania kutoa elimu kuhusu utekelezaji wa majukumu yake na dhana nzima ya udhibiti, Pamoja na kutoa elimu kwa umma kwa ujumla, msukumo wa elimu hii pia unawalenga viongozi serikalini na wadau wengine.

Programu hii imeanzia katika Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kwa mwaka wa Fedha wa 2018/2019. Ofisi ya EWURA ya Kanda ya Ziwa ina hudumia mikoa saba ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Geita, Simiyu na Kigoma.

Kwa mujibu wa maelezo ya Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano kutoka EWURA, Titus Kaguo anasema kama ilivyoaanishwa katika Sheria ya EWURA kipengere cha 6 (e, moja ya majukumu ya EWURA ni kutoa elimu kwa wadau wake kuhusu kazi na majukumu ya Mamlaka kwa sekta inazozidhibiti.

Anaesema Elimu hutolewa kwa kutumia njia mbalimbali za mawasiliano kama luninga, magazeti, redio na mitandao. Hata hivyo, pamoja na kutumia njia hizo zote za mawasiliano,Elimu kwa Umma kwa sehemu kubwa imekuwa ikitekelezwa vizuri kwa ngazi ya kitaifa kupitia kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma Makao Makuu. Hata hivyo, Ofisi za Kanda zinawajibu pia wa kutoa elimu kwa wadau wake kwa ushirikiano na kitengo cha Mwasiliano makao makuu.

Kaguo anasema ifahamike kuwa, wadau wa EWURA ni pamoja na watoa huduma zinazodhibitiwa na EWURA, watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji, Wizara, Idara za Serikali, Mashirika ya Umma, Serikali za Mitaa, Vyama vya Kiraia, Vyombo vya habari, Wabia wa Maendeleo, Wawekezaji, Wanasiasa na wananchi kwa ujumla.

Mkakati wa elimu kwa umma ulivyowafikia wahariri wa vyombo vya habari

Kaguo anaeleza kuwa EWURA imekutana na wahariri wa vyombo vya habari nchini katika jitihada zake za kufikisha elimu kwa wadau mbalimbali na umma kwa ujumla juu ya masuala ya udhibiti.

“Katika mkutano huo, wahariri wote kutoka vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo, Televisheni, redio, magazeti na habari za mtandao walipata wasaa wa kusikiliza wasilisho kutoka kwa Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano kutoka EWURA, ambaye ni yeye Titus Kaguo lililohusu, kazi, wajibu na changamoto mbalimbali zilizoikabili taasisi katika kipindi cha mwaka 2018/2019, pamoja na mipango mikakati ya mbeleni ya Mamlaka.

“EWURA ni mdhibiti wa huduma za nishati na maji, ambazo humgusa moja kwa moja, mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi pamoja na watoa huduma hivyo basi kupitia wahariri na vyombo vya habari ni rahisi kufikisha taarifa muhimu kwa wananchi hao.

“Ninyi ni mabalozi wetu muhimu katika kuhakikisha taarifa zinawafikia wananchi katika muda muafaka, hivyo basi, tumeona tukutane nanyi, ili mpate kufahamu masuala muhimu ya kiudhibiti na kuifahamu taasisi yetu vizuri ili mwende kuelimisha umma juu ya kazi na wajibu wetu,” anasema .

Aidha anasema kuwa EWURA itaendelea kuboresha ushirikiano na wahariri pamoja na waandishi wa habari, ili kuongeza uwazi katika kufanya kazi zake na kuwahabarisha wananchi moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji miradi ya umeme

Anasema ili kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi kwenye uwekezaji wa miradi midogo ya kuzalisha umeme (chini ya Megawati 10), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) iliandaa mikataba elekezi ya kuuziana umeme (Model Power Purchase Agreements) kati ya TANESCO na wawekezaji.

“Mikataba hii, pamoja na masuala mengine hupunguza muda wa majadiliano kati yao na inawezesha uwekezaji na utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

“EWURA imetayarisha bei elekezi za ufuaji umeme utokanao na maji, gesi asilia, makaa ya mawe, jotoardhi, umeme wa jua, upepo na mafuta ili kuiwezesha Tanzania kuwa na umeme wa uhakika kwa matumizi ya viwanda.

“Hatua hizi ni sehemu ya jitihada kubwa zinazofanywa na EWURA katika kuimarisha mazingira ya kuvutia uwekezaji katika miradi ya umeme ili kushajihisha utekelezaji wa sera ya viwanda.

“Mamlaka imeendelea kuratibu mabadiliko katika sekta ndogo ya umeme (ESI) ambayo yanalenga kuongeza uwezo wa uzalishaji kufikia Megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.

“Aidha, katika kutekeleza majukumu yake ya kiudhibiti, EWURA imeboresha huduma za utoaji leseni za umeme kwa kuimarisha mfumo wa uombaji leseni kwa njia ya mtandao yaani LOIS, upangaji wa bei pamoja na kusimamia ubora wa huduma zinazotolewa” anaeleza Kaguo.

EWURA kukabiliana na mafundi umeme wasiyo na leseni ya Mamlaka hiyo

Kwa maelezo ya Kaguo anasema EWURA imetoa onyo kwa mafundi umeme wote wanaofanya shughuli za ufungaji wa mifumo ya umeme, bila kuwa na leseni hai iliyotolewa na EWURA.

Pia anasema EWURA inatoa tahadhari kwa mafundi umeme wanaotoa huduma za uwekaji mifumo ya umeme, bila kuwa na leseni halali, kuacha mara moja na kuomba leseni itakayo waruhusu kufanya shughuli hizo EWURA.

“Kwa mujibu wa sheria ya umeme, kazi zote za ufungaji umeme, ikiwemo upanuzi, kubadili, kufanya marekebisho na matengenezo kwenye mifumo, zinatakiwa zifanywe na fundi mwenye leseni iliyotolewa na EWURA. ili kuhakikisha shughuli hizo zinaendeshwa na watu wenye utaalamu stahiki kwa usalama wa watu na mali zao.

“EWURA inawatahadharisha wateja wa huduma za uwekaji mifumo ya umeme kuepuka kutumia mafundi wasiokuwa na leseni. Kwa utambuzi ni vyema kuomba kitambulisho cha fundi husika au kutumia orodha ya mafundi inayopatikana kwenye tovuti ya EWURA www.ewura.go.tz.

“Kwa mantiki hiyo ni kosa la jinai kuendesha shughuli za ufungaji umeme bila kuwa na leseni halali, mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuendesha shughuli hizo bila leseni atatozwa faini ya shilingi milioni tano au kifungo cha miaka mitano au adhabu zote kwa pamoja.

“Mpaka mwishoni mwa mwezi Machi 2019, jumla ya leseni zaidi ya 1,000 zilikuwa zimetolewa kwa mafundi umeme Tanzania bara hivyo, ni kosa kisheria kufanya shughuli za ufungaji umeme, bila ya kuwa na leseni ya EWURA, Mtu yeyote akikamatwa na kosa hilo atapata adhabu ya kulipa faini au kifungo cha miaka mitatu jela.

EWURA yazipiga msasa Mamlaka za maji

Katika kuimarisha utoaji huduma za maji na usafi wa mazingira kwa wananchi, EWURA imekuwa ikikutana na Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuhakiki taarifa zao za utekelezaji wa majukumu ili kuiwezesha EWURA kuandaa taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka.

Kwa Mujibu wa taarifa ya Kaguo inasema Mpango wa Mamlaka  ni kupima utendaji kazi ukiwa wa uwazi na umelenga kuhakikisha Mamlaka zinaimarisha ukusanyaji mapato, utoaji huduma na kuzingatia viwango vya ubora.

EWURA ilivyong’ara tuzo za NBAA 2017

Mwaka 2017, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilishinda tuzo ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), kwa kuwa mshindi wa pili katika uandaaji na uwasilishaji bora zaidi wa taarifa ya fedha, kwa mwaka 2017.

Tuzo hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashatu Kijaji katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi cha NBAA, Bunju, Dar es Sar es Salaam na kupokelewa na Mkurugenzi wa Fedha, Rasilimali Watu na Utawala wa EWURA, Stanley Mahembe.

Kwa taarifa kutoka EWURA zinazsema kuwa ushindi huo umetokana na kufuata miongozo ya kitaifa na kimataifa katika uandaaji wa hesabu pamoja na kutoa maelezo ya ziada yanayofafanua vizuri zaidi na kwa undani hesabu na utendaji kazi wa Mamlaka.

EWURA ni mongoni mwa taasisi tatu bora kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa Mamlaka nchini, kwa mujibu wa ukaguzi uliofanywa na NBAA kwa mwaka 2017.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!