MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeshindwa kutoa hukumu ya rufaa ya Serikali dhidi ya Sheikh Issa Ponda kwa mara nyingine, anaandika Faki Sosi.
Katika rufaa hiyo Serikali inapinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro iliyomuachia huru Sheikh Ponda katika tuhuma ya uchochezi.
Hukumu hiyo iliyotarajiwa kutolewa jana na Jaji Mkasi Mongwa ambaye amesema ameshindwa kutoa hukumu hiyo kwa kuwa hajamaliza kuianda na badala yake ataitoa Novemba 23, mwaka huu.
Inatarajiwa kwenye hukumu hiyo endapo Jaji Mongwa anayesikiliza shauri hilo ataridhika na madai ya upande wa Serikali, Sheikh Ponda atatiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu.
Kama Jaji hataona ukweli katika madai ya Serikali, atatupilia mbali rufaa hiyo na kumuachia huru Sheikh Ponda.
Leave a comment