Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Huko twitter, Nape hapumui
Habari za Siasa

Huko twitter, Nape hapumui

Spread the love

NAPE Nnauye, Mbunge wa Mtama mkoani Lindi, mara kadhaa aandikapo kwenye ukuraswa wake wa twitter, ujumbe wake huzua mjadala na kurejelea kauli yake ya ‘bao la mkono.’ Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Andiko aliloweka kwenye ukurasa wake ‘Raha ya Kushindana, Kushinda,! limezua mjadala huku akilazimika kujibu baadhi ya shutuma zinazoelekezwa kwake.

Andiko hilo aliliweka tarehe 5 Novemba 2019, wakati ambao kuna malalamiko kwa wasimamizi wa uchaguzi kubagua wagombea wa vyama vya upinzani, na kutaka CCM ipite bila kushindana.

Mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Descanius J. William, alimuhoji Nape kwamba kwa nini, hakulijua suala hilo, enzi za goli la mkono?

Kutokana na swali hilo, Nape alimjibu William kwa kumuuliza swali “goli hilo lilikuuma eeeeh?”

Kwenye mjadala huo, mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Yule_Boy ameandika, kwamba Nape ni msema kweli lakini mnafiki,“msema kweli we ila shida yako mnafiki sanaaa.”

Kutokana na ujumbe huo, Nape alimjibu “Kama mie mnafiki na bado unaendelea kuni-follow- basi we mzandiki!” baada ya ujumbe huo, Peterleah18 nayee aliandika “na mwisho wenu utafika tu.”

Mwenye utambulisho wa jina la Mjukuu, aliandika kwenye ukurasa huo wa Nape kwamba, “sio bure ulienda kulialia adi ukasamehewa, angemwaga unga na mboga kabisaa.. ushaandaliwa kushinda sasa.”

Mchangiaji Angry Citizen kwenye mjadala huo aliandika “CCM hawataki kushindana sio kwa hoja hata kwa kura. Sasa sijui hizo ruzuku wanazitoa kwa vyama za kazi gani?”

Naye Fredrick Justine, alimshauri Nape, kwamba ushauri wake aufikishe kwenye mamlaka husika.

Asombwile David, alimweleza mbunge huyo wa Mtama kumsaidia mbinu Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alizotumia na Mzee Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu Mstaafu, kukipa ushindi chama chao.

Kufuatia mjadala huo, Nape alijibu kwa kuandika kwamba, vyama vya upinzani haviweki wazi kiini cha changamoto zao. Na kwamba makosa ya upinzani ni kuainisha mambo ambayo sio chanzo cha tatizo.

“Moja ya makosa ya upinzani unafanya ni kujaribu kuadress jambo ambalo kimsingi sio chanzo cha tatizo na kuacha tatizo lenyewe,” ameandika Nape.

Pip Haule akichangia mjadala huo aliandika “Nape bora unyamaze….tunawaheshimu tu kwa sababu ni watu wazuri lakini nyie na mzee wetu Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) ndo mlioleta hizi shida.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!