Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hospitali ya Uhuru yapokea wagonjwa wa nje
Habari za Siasa

Hospitali ya Uhuru yapokea wagonjwa wa nje

Spread the love

HOSPITALI ya Uhuru, Dodoma inayojengwa kwa gharama ya Sh. 3.9 Bilioni, imeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17 Januari 2021, na Dk. Eusebius Kessy ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo.

“Hospitali yetu imeanza kutoa huduma tangia tarehe 21 Desemba 2020, na mpaka sasa imeshahudumia wateja takribani 300,” amesema Dk. Kessy.

Amesema, ujenzi wa hospitali hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Chamwino na maeneo ya karibu na kwamba, watahahakisha huduma zinakuwa bora kama ilivyokusudiwa.

Dk. kessy amesema, hospitali hiyo inatoa huduma kwa wagonjwa wenye Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na pia wale ambao hawana bima ya afya.

Akizungumzia huduma zinazotolewa kwa sasa amesema, kuna huduma za maabara, klinik za macho na meno, mionzi, klinik za mama na mtoto na huduma za wagonjwa wa nje (OPD).

Meshack Bandawe, Katibu wa Kuratibu Shughuli za Serikali kuhamia Dodoma ambaye alifanya ziara maalum kukagua maendeleo ya hospitali hiyo amesema, ujenzi wa hospitali hiyo umekamilika kwa asilimia 99.8.

Amebainisha kuwa, maagizo yaliyotolewa na Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu alipofanya ziara tarehe 20 Novemba 2020, yametekelezwa ikiwemo kukamilisha ujenzi wa jengo ifikapo tarehe 5 Desemba 2020, vigae vya chini, miundombinu muhimu na ukamilishaji wa ukuta kuzunguka hospitali hiyo ambao umekamilika kwa asilimia 99.

Pamoja na hayo amesema mifumo ya maji na umeme na miundombinu mbalimbali imekamilika pamoja na vifaa tiba vya Utra sound, X-ray,ECG na baadhi ya samani ambavyo vimeshawasili hospitali hapo.

Amesema, Siku ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kulifanyika uchangiaji wa damu salama na kufanikiwa kupata unit 48 za damu.

Aidha, amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia SUMA JKT ambao ndio mkandarasi wa hospitali hiyo, mshauri mwelekezi wakala wa majengo Tanzania (TBA), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa usimamizi wa ujenzi wa hospitali hiyo.

Ujenzi wa Hospitali ya Chamwino ulitokana na agizo la Rais John Magufuli kwamba, fedha zilizotengwa kwa ajili ya Sherehe ya Miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara (9 Desemba 2018), zitumike kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!