Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Hospitali ya Benjamini Mkapa yaanza kutibu ugonjwa wa selimundu
Afya

Hospitali ya Benjamini Mkapa yaanza kutibu ugonjwa wa selimundu

Hospitali na Benjamini Mkapa ya Dodoma
Spread the love

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Magonjwa ya Kibingwa ya Benjamini, Dk. Alphonce Chandika amesema, hospitali hiyo inatarajia kuanza kutibu ugonjwa wa selimundu kwa kupandikiza uume usiokuwa na maambukizi ifikapo mwaka 2020. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Alitoa kauli hiyo wakati akzingumza na waandishi wa habari kusiana na matibabu ya ugonjwa huo ambao alisema unawatesa watoto wananozaliwa na ugonjwa huo kwa kumfanya mgonjwa kupata maumivu makali ya mara kwa mara na matibabu yake licha ya kuwa ni gharama lakini anatakiwa kutibiwa maisha yake yote ya mgonjwa.

Dk. Chandika alisema, takwimu zilizopo zinaonyesha katika zima la Afrika lina vituo 10 tu vinavyotoa huduma hiyo ambapo sita vipo Afrika Kusini, kituo kimoja kipo Nigeria, Misri na Tunisia na kwa Afrika Mashariki hakuna kituo hata kimoja hivyo Benjamin Mkapa kitakuwa kitiuo cha kwanza Afrika Mashariki.

”Kupata huduma hii ni fursa kubwa na muhimu kwetu, maana sote tunafahamu magonjwa ya selimundu na saratani ya damu kwamba, matibabu yake ni kufanya upandikizaji ya uume, sasa tumejipanga ifikapo mwaka 2020 kuanza kutoa huduma hii na tutaanza na huduma ya kuwasidia watoto wenye selimundu,” alisema Dk. Chandika

Alisema, suluhisho la  kudumu la ugonjwa huo ni kufanya upandikizaji wa uume kwa  kuuondoa unaozalisha chembe chembe  za damu ambazo siyo nzuri na kuwekewa mwingine ambao utazalisha damu ambayo haina chemchembe za ugonjwa wa selimundu na mgonjwa anapona kabisa.

Akitoa takwimu zilizotolewa na taasisi zinatoa huduma hiyo ambazo siyo rasmi alisema, inasadikika kwamba, kwenye kundi la watoto 100 wanaozaliwa, mtoto mmoja anakuwa na ugonjwa huo.

Aidha alisema, kila mwaka kuna takribani wagonjwa 20,000 wanaugua ugonjwa huo ambapo kila mwaka nusu ya wagonjwa hao wanaishia kupoteza maisha.

“Licha ya kuwa takwimu hizo siyo rasmi lakini  tatizo ni kubwa na idadi hiyo ni kubwa sana, hivyo kwa kuanzisha huduma hii tutaokoa maisha ya watanzania wengi wanaougua ugonjwa huu,” alisema Dk. Chandika na kuongeza kuwa;

”Huu ni mwanzo na tunaanza kwenda, siyo stori kwenye vyombo vya habari, tunamaanisha na tumedhamiria, lakini pia ni katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015.”

Kwa upande wake Prof. Cornelio Uderzo kutoka San Grvardo hospitali ya Chuo Kikuu cha Monza nchini Italia ambaye amefika katika hospitali ya Benjamini Mkapa kama sehemu ya maandalizi ya awali katika kuangalia miundombinu na mahitaji yanayohitajika  alisema, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoendelea zilizoanza kutoa matibabu hayo.

Kwa mujibu wa Profesa huyo, kwa mwaka huu wanaanza kujenga uwezo kwa timu ya madaktari wa kutoa huduma hiyo.

Kwa upande wake, Daktari bingwa wa watoto katika hsopitali hiyo Dk. Shgakilu Jumanne alisema, matibabu ya ugonjwa huo ni muhimu ili kuzuia magonjwa mengine yanayoambatana nao na kumsababishia mgonjwa adha.

Alisema kadri magonjwa ya seli ya damu yanavyoendelea kama selimundu, unaathiri moyo, figo, maini, lakini pia unatengeza mawe kwenye maini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!