Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Hospitali matatani kwa kumuambukiza mgonjwa VVU
Kimataifa

Hospitali matatani kwa kumuambukiza mgonjwa VVU

Jengo la hospitali ya Pinderfields. Picha ndogo kitanda kilichokuwa na damu ya mgonjwa wa ukimwi
Spread the love

HOSPITALI moja nchini Uingereza inayofahamika kwa jina la Pinderfields imeingia matatani baada ya kutuhumiwa kutaka kumsabishia mgonjwa Paul Batty (52) kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Batty aliyelazwa hospitalini hapo wiki mbili zilizopita, alilazimika kupima mara kadhaa hospitalini, ili kubaini kama amepatwa na maambukizi ya VVU baada ya kugundua kwamba kitanda alicholalia ndani ya saa 24 wakati alipolazwa hospitalini hapo, kilikuwa na damu ya mgonjwa mwengine.

Batty ambaye ni mkazi wa kijiji cha Fitzwilliam mjini Yorkshire nchini Uingereza alieleza kuwa, anatakiwa kurudi hospitalini miezi mitatu baadae ili apime kama hajapata maambukizi ya VVU na Hepatitis A na B baada ya vipimo vya awali kugundua kwamba hajaathirika.

Akielezea jinsi alivyogundua tukio hilo, Batty aliyeifananisha hospitali hiyo na Jehanam, alisema binti wa rafiki yake aliyemtembelea hospitalini hapo pamoja na mkewe, ndiye aliyeona na kueleza kuhusu uwepo wa damu ya mgonjwa mwengine chini ya kitanda.

Kufuatia tukio hilo, Hospitali ya Mid Yorkshire NHS kwa niaba ya hospitali ya Pinderfields ilimuomba radhi Batty huku ikikiri kuwa, kuna uzembe uliofanywa na baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo kwa kutosafisha kitanda hicho kwa wakati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!