Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hoja ya Uchaguzi Mkuu 2020 yaibuka msiba wa Mkapa
Habari za Siasa

Hoja ya Uchaguzi Mkuu 2020 yaibuka msiba wa Mkapa

Adam Kimbisa, Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Spread the love

VIONGOZI mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania, wameendelea kujitokeza nyumbani kwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa nchi hiyo, Benjamini William Mkapa, Masaki jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu,Dar es Salaam … (endelea).

Mkapa aliyeongoza Tanzania kati ya tarehe 23 Novemba 1995 hadi 2005 alifikwa na mauti usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa Mkapa utaanza kuagwa kesho Jumapili hadi Jumanne tarehe 28 Julai 2020 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kasha utasafirishwa kwenda kijijini kwake Lupaso, Masasi Mkoa wa Mtwara kwa maziko yatakayofanyika Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020, wanasiasa waliofika msibani, wametoa wito kwa Watanzania kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, unakuwa wa amani na utulivu, ili kumuenzi kiongozi huyo mstaafu.

Adam Kimbisa, Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, amesema Tanzania itaukosa ushauri muhimu wa Mkapa, katika uchaguzi mkuu ujao.

“Tutamkumbuka kwenye uchaguzi huu sababu siku za kufunga kampeni ama kufungua anakuwa msemaji mzuri wa kututia moyo. Lakini ameweka mfumo mzuri. Kwenye uchaguzi alituwekea utaratibu mzuri wa kuweka kampeni za kistaarabu,” amesema Kimbisa.

 

Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana

Naye Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema hakuna uchaguzi rahisi.

Kinana amesema, uchaguzi sio rahisi, kushinda kwa kuwa kura haiko katika midomo ya watu, bali iko katika mioyo yao.

“Hakuna uchaguzi rahisi, sababu kura haiko kwenye midomo ya watu iko kwenye mioyo ya watu. Hivyo, uchaguzi unataka mipango, yataka mikakati ya ushawishi kujua watu wanataka kitu gani ili wawachague,” amesema Kinana.

Kinana amesema, enzi za uhai wake, Mkapa alifanya kazi kubwa kutengeneza marais wawili, Jakaya Mrisho Kikwete aliyemwachia madaraka mwaka 2005 na John Pombe Magufuli aliyeingia madarakani tarehe 5 Novemba 2015 kutoka kwa Kikwete.

George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani

“Alipostaafu, alikuwa anaendelea kutoa mchango na aliwezesha Kikwete kushinda uchaguzi. Alifanya kazi kubwa kutengeneza marais wawili, Rais Kikwete na Rais Magufuli,” amesema Kinana.

Kwa upande wake, George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani amesihi Watanzania kutotofautiana katika uchaguzi huo ili Tanzania iendelee kubaki na amani, iliyotunzwa na marais wastaafu, akiwemo Mkapa.

“Wito wangu kwa Watanzania, tushirikiane katika kuomboleza, tutafakari maisha yetu kama Taifa tunapopoteza mmoja wapo lazima tutafakari hasa kipindi hiki tunachokwenda katika uchaguzi. Tusipigane maana wazee wameondoka wametuachia nchi nzuri ambayo kila mtu anaishi vizuri,” amesema Simbachawene.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!