Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Hivi ndivyo Sheikh Ponda alivyokamatwa msikitini
Tangulizi

Hivi ndivyo Sheikh Ponda alivyokamatwa msikitini

Sheikh Issa Ponda, Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu
Spread the love

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, amekamatwa na polisi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Tukio la kukamatwa kwake lilitokea juzi jioni tarehe 11 Julai 2020, alipokuwa ofisini kwake katika Msikiti wa Bungoni, jijini Dar es Salaam. 

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amethibitisha kumshikilia Sheikh Ponda akisema, wanamuhoji kwa madai ya kufanya uchochezi katika waraka wake.

“Tunaye sisi polisi, tumemkamata kwa mahojiano ya uchochezi walioutoa kwenye kitu walichokiita waraka, hivyo tunamhoji kutokana na ule waraka,” amesema Mambosasa.

Kwenye waraka huo uliosomwa na Sheikh Ponda Issa Ponda, tarehe 9 Julai 2020 jijini Dar es Salaam, miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye waraka huo ni pamoja na kuitaka serikali kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu unakuwa huru na haki, pia umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya.

“Kwa hakika maelezo yetu ya nini tunataka kwa taifa letu katika uchaguzi huu, yangekuwa na maana sana kama Taifa lingekuwa na Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Tume Huru ya Uchaguzi, vinavyotokana na Wananchi wenyewe,” alisema Sheikh Ponda.

Taarifa kutoka kwa Ibahim Mkondo, katibu wa sheikh huyo akizungumzia alivyokamatwa Sheikh Ponda ameeleza, baadhi ya polisi walivaa kiraia na wengine walivaa sare na kwamba, baadhi walibaki nje na wengine waliingia ndani kumtafuta.

“Walioingia ndani walikuwa hawamfahamu Sheikh Ponda, walipofika ndani, walimkuta mtu tunayemwita Yasin Kazinyingi na walitaka ajitambulishe. Alipojitambulisha, wakasema huu sie.

“Wakauliza kama kuna mtu mwingine ndani, kisha wakaingia, wakamkuta Sheikh Ponda kisha wakamwambia kuna mahojiano, hivyo anatakiwa kwenda naye Kituo cha Polisi cha Kati, walimchukua na kuondoka naye,” amesema Ibrahim.

Anasema, polisi waliongia ndani kumtafuta Sheikh Ponda walikuwa wamevalia kiraia, ‘ndani waliingia kama askari sita,” amesema.

Na kwamba, baada ya kukamatwa, familia yao ilipata taarifa na kuwa, saa mbili usiku walimpeleka chakula katika Kituo cha Polisi cha Kati.

“Kulikuwa na mahojiano kati ya polisi na waliopeleka chakula, wakati mahojiano yakiendelea, walimuona Sheikh Ponda anatolewa ndani kituoni na kuingizwa kwenye gari.

“Kuna mtoto wake mmoja wa kike aliita kisha polisi wakasimamisha gari, mtoto wake wa kiume alichukua kile chakula na kukipeleka kwa baba yake, kikapokelewa. Hapo tulikuwa Kituo cha Kati,” amesema Ibrahim.

Amesema, jana tarehe 12 Julai 2020, walipokwenda kwenye Kituo cha Polisi cha Kati waliambiwa hayupo, kisha walikwenda Kituo cha Polisi Kigogo (Mburahati), wakaambiwa hayupo na pia walikwenda kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay ambapo napo waliambiwa hayupo.

Licha ya Jeshi la Polisi kuthibitisha kumkamata Sheikh Ponda, lakini anasema mpaka sasa hawana taarifa kituo alipo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda kung’oka tena

Spread the loveUWEZEKANO wa Paul Makonda, kuendelea na wadhifa wake wa mkuu...

error: Content is protected !!