Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Hiki ndicho kilichomuondoa Kocha Mwinyi Zahera Yanga
Michezo

Hiki ndicho kilichomuondoa Kocha Mwinyi Zahera Yanga

Spread the love

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umetangaza kuachana na kocha wake, Mwinyi Zahera baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hizi ndiyo sababu za klabu hiyo kufikia maamuzi hayo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Sababu ya kwanza ni kiwango cha timu kilichooneshwa katika michezo ya hivi karibuni ya kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na ile michezo ya kimataifa baada ya timu kuonekana kushindwa kutengeneza nafasi za mabao katika safu yake ya ushambuliaji licha ya kusajili wachezaji sita wapya katika eneo hilo.

Eneo lingine ambalo kocha Zahera alisindwa ni kuifanya timu kuwa na muunganiko kutokana na kusajili wachezaji takribani 15 wapya kwenye kikosi hicho na kushindwa kuipanga timu jambo ambalo liliighalimu sana Yanga kwenye baadhi ya michezo mpaka kupelekea kupoteza.

Toka msimu huu uanze hivi karibuni, Zahera amecheza jumla ya michezo 10, ikiwa minne ya Ligi Kuu  na sita ya michuano ya kimataifa na kati ya hiyo ameshinda michezo mitatu, amefungwa michezo minne na kwenda sare mechi tatu.

Pengine zinaweza zisiwe takwimu mbaya kwake licha ya ligi bado kuwa mbichi kwa kuwa mpaka sasa amecheza michezo minne lakini kilichoweka wasiwasi mkubwa ni aina ya mchezo wanaoonesha wakiwa uwanjani kama timu kwa kuwa mara nyingi wanakuwa wamezidiwa muda wote wa mchezo.

Sababu zote juu zingeweza kuvumilika na hata kumpa muda ili timu ikae sawa lakini swala lililomuweka pabaya zaidi ni aina ya matamko aliyokuwa akiyatoa kwa mashabiki baada ya kuhoji timu yao kutocheza vizuri katika mchezo waliopoteza wakiwa nyumbani dhidi ya Pyramids kwenye michuno ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Zahera angeweza kuwajibu kuifundi zaidi kuliko kuliko kusema yale aliyozungumza kuwa walikuwa hawawezi kuwafunga Pyramids kwa kuwa wamewazidi kila kitu na hakuna hata mchezaji wake hata mmoja ambaye anaweza kucheza kwenye ile timu.

Ikumbukwe Zahera aliingia Yanga aprili 28, 2018 na kusaini mktaba kama kocha mkuu na kufanikiwa kuiongoza Yanga kwa jumla ya michezo 63 amefanikiwa kushinda mechi 32 na kupoteza 21 na kwenda sare michezo 10 na katika michezo yote hiyo walifanikiwa kushinda jumla ya mabao 58 na kufungwa mabao 71.

Kwa sasa nafasi ya kocha huyo inachukuliwa na Boniface Mkwasa ambaye atakaimu kwa muda huku uongozi wa klabu hiyo ukiendelea na mchakato wa kumtafuta kocha mkuu atakaye kinoa kikosi hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!