Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hazina waisusia mishahara Lushoto
Habari za Siasa

Hazina waisusia mishahara Lushoto

Angela Kairuki, Waziri wa Madini
Spread the love

HALMASHAURI ya wilaya ya Lushoto inatumia zaidi ya Sh. 28 milioni kulipa mishahara ya watumishi kila mwezi Bunge limeelezwa, anaandika Dany Tibason.

Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali Bungeni ambapo amesema huo ni mzigo kwa Halmashauri ambapo kazi hiyo ilipaswa kufanywa na Hazina kupitia Utumishi.

“Je, ni lini Serikali itawatua wananchi wa Lushoto mzigo huo?” alihoji Shangazi

Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angela Kairuki almesema katika Halmashauri ya wilaya wapo watumishi wanaolipwa kutoka Serikali Kuu na watumishi wanaolipwa kutoka katika vyanzo vya Mapato ya ndani ya halmashauri husika ‘own source’.

Amesema utaratibu huo ulianzishwa baada ya kuonekana kuwepo kwa mahitaji maalum yanayowasilishwa na waajiri kutaka watumishi wa ziada tofauti na ukomo wa bajeti ya mishahara ya serikali.

Kairuki amesema Halmashauri ya Lushoto inao mzigo huo kwa kuwa iliona inao uwezo wa kuwalipa watumishi wake kupitia Mapato yake ya ndani.

“Kwa upande wa Halamshauri ya Lushoto kuna jumla ya watumishi 116 ambao waliajiriwa katika utaratibu huo ‘own source ‘ kwa kuwa halmashauri hiyo ilitoa inaweza kumudu gharama za kuwalipa mishahara kutokana na vyanzo vyake vya mapato ya ndani,” amesema Kairuki

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!