Tuesday , 19 March 2024
Home Kitengo Michezo Hatma ya Lulu kubaki uraiani au lupango, yamebaki masaa
MichezoTangulizi

Hatma ya Lulu kubaki uraiani au lupango, yamebaki masaa

Elizabeth Michael (Lulu) akitokea katika Mahakama Kuu
Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam kesho inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya kuua bila kukusudi inayomkabili Msanii wa filamu Elizabeth Micheal, (Lulu), anaandika Faki Sosi.

Lulu anatuhumiwa kuwa Aprili 7, 2012 alimuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba bila ya kukusudia, Jaji Sam Rumanyika ndiye atakayetoa hukumu hiyo kesho.

Endapo Jaji atamkuta Lulu hana hatia atamuacha huru na akimkuta na hatia ya kuua bila kukusudia adhabu za makosa hayo hutofautiana kutokana na mazingira ya tukio jinsi lilivyotokea, ushahidi uliowasilishwa mahakamani na mwenendo wa kila siku wa mtuhumiwa.

Rekodi ya mtuhumiwa itazingatiwa kwenye hukumu hiyo kama alishawahi kufanya kosa kama hilo au makosa mengine kipindi cha nyuma pamoja na tabia zake kiujumla.

Upande wa Jamhuri ulileta mahakamani mashahidi wanne wakiwemo Seth Bosco ambaye ni mdogo wake Marehemu Kanumba, waliokuwa wakiishi kwenye nyumba moja na marehemu na alikuwepo siku ya tukio, Dk. Paplas Kagaiga aliyekuwa Daktari wa familia hiyo ambaye aliyefika nyumbani kwa Marehemu Kanumba mara baada ya kudondoka.

Wengine ni Daktari kutoka kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Marehemu Kanumba pamoja askari ASP Ester aliyefanya upelelezi kwenye tukio hilo pamoja na kumtia mbaroni Lulu.

Lulu aambaye anatetewa na wakili Peter Kibatala, waliwasilisha mashahidi wa wawili ambao ni Lulu mwenyewe aliyehadithia mazingira ya tukio na kueleza kuwa hakuhusika kwa namna yoyote kwenye kifo cha Marehemu Kanumba.

Mbivu na mbichi kwenye kesi hii tutajua kesho saa 3 asubuhi kwenye Mahakama Kuu, MwanaHALISI Online itakujuza kila kitakachotokea katika hukumu hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

CDF Mabeyo: Magufuli alijua anakufa

Spread the love  ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi nchini (CDF), Jenerali Venance Mabeyo,...

AfyaTangulizi

Serikali yafafanua kuondolewa dawa 178 kitita cha NHIF

Spread the loveSERIKALI imesema imeondoa dawa 178 katika kitita cha Mfuko wa...

error: Content is protected !!