January 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hatma Mdee na wenzake leo, wanachama wajitokea makao makuu

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo Ijumaa tarehe 27 Novemba 2020, kinafanya kikao maalum cha kamati kuu kuwajadili wanachama wake 19 wanaodaiwa kukisaliti kwa kukubali uteuzi wa ubunge viti maalumu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kikao hicho, kinafanyika jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Wanachama hao 19 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee wanajadiliwa baada ya tarehe 24 Novemba 2020 kwenda bungeni jijini Dodoma kuapishwa na Spika Job Ndugai.

Kutokana na tuhuma hizo za usaliti, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alitangaza kufanyika kwa kamati kuu leo Ijumaa na kuwataka kufika makao makuu ya Chadema, Kinondoni Dar es Salaam saa 2:00 asubuhi.

Hata hivyo, MwanaHALISI Online limefika makao makuu ya chama na kukuta baadhi ya wanachama wakiwa na mabango mbalimbali yanayoishauri kamati kuu kuwafukuza Mdee na wenzake 19.

Hadi saa 4:30 asubuhi, Mdee na wenzake walikuwa hawajafika huku MwanaHALISI Online likidokezwa kwamba “wameleta barua ya kutojadiliwa wakiomba kikao kisogezwe mbele.”

“Unaweza kujiuliza kwa nini wote 19 walete barua ya kuomba udhuru, bora wangekuja hata watano wengine wakaomba udhuru huo, sasa wote 19 kweli, haya ni makusudi,” amedokeza mmoja wa wajumbe wa kamati kuu.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Mnyika amesema, kikao kinafanyika leo Ijumaa kama kilivyopangwa.

“Naomba nisizungumze chochote kuhusu hilo, kwa sasa naelekea katika kikao cha kamati kuu ya chama. Tutakapokiwa tayari kuongea na wanahabari tutazungumza lakini kwa sasa tunaelekea katika kikao cha kamati kuu,” amesema Mnyika.

Mbali na Mdee, wengine ni; Ester Bulaya na Esther Matiko ambao ni wajumbe wa kamati kuu. Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Nusrat Hanje. Katibu Mkuu Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), na Grace Tendega.

Makamu Mwenyekiti Bawacha, Hawa Mwaifunga. Naibu Katibu Mkuu Bawacha, Jesca Kishoa  na Katibu Mwenezi Bawacha, Agnesta Lambat.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Mtwara, Tunza Malapo. Ceciia Pareso. Asia Mwadin Mohamed. Felister Njau. Naghenjwa Kaboyoka. Sophia Mwakagenda. Kunti Majala. Stella Siyao.Salome Makamba. Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Wakizungumza na Mtandao huu baadhi ya wanachama waliofika makao makuu ya Chadema kishuhudia mchakato huo, wameshauri Kamati Kuu kuwafukuza uanachama.

“Kina Halima itawagharimu, machozi ya wanawake yatawatafuna hususan kwa jinsi tulivyopambana wanakuja kutusaliti kama chama. Machozi ya wanawake yatawagharimu,” amesema Monica Azaria, Mwenyekiti wa Bawacha Kibamba, Dar es Salaam.

NayeVeronica Mwanjala, aliyekuwa  Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia Bawacha amesema “tumeumziwa sana na watu wanaosaliti, tunajua Mdee alishawishiwa kwa kiasi.”

“Kikubwa, tunaiomba kamati kuu iwaondolee uanachama wote pia wapo waliowashawishi ndani ya kamati kuu wachukuliwe hatua,” amesema.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!