Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Halima Mdee: Lowassa anavuja damu ya usaliti
Habari za SiasaTangulizi

Halima Mdee: Lowassa anavuja damu ya usaliti

Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu
Spread the love

HATUA ya Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema kurejea CCM imetajwa kwamba ni usaliti kwa waliomwamini na kumpigia kura kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe amesema, Lowassa ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amelazimika kurejea CCM kutokana na kuelemewa na changamoto nyingi za kibiashara na kifamilia.

Mdee ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Machi 2019 kupitia andiko lake aliloandika katika ukurasa wake wa Twitter baada ya watu kuhoji ukimya wake kuhusu tukio la kuhama kwa Lowassa.

Aidha, Mdee ameeleza kuwa, anajua kwamba nafsi ya Lowassa inavuja damu ya usaliti kwa wananchi waliompigia kura za urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Natambua changamoto nyingi anazopitia za kifamilia na kibiashara, akalazimika kuomba po! sikuona haja ya kusema chochote nikiheshimu uamuzi wake.

“Najua nafsi yake inavuja damu ya usaliti kwa waliompa heshima na ‘kumrudishia uhai’(wananchi waliompigia kura nyingi sana)!,” ameandika Mdee.

Mdee amendika kuwa, hakuona haja ya kusema chochote kuhusu hatua ya Lowassa kurejea CCM, kwa sababu ameheshimu uamuzi wake.

Lowassa alirejea CCM tarehe 1 March 2019 akipokewa na Dk. Magufuli, Mwenyekiti wa CCM Taifa. Kwenye mapokezi hayo, Lowassa alizungumza maneno machache kwamba “nimerudi nyumbani.”

Pia alipokewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa chama hicho katika ofisi ndogo za CCM zilizoko Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!