‘Hakuna atakayejifungua kwa shida’

Spread the love

“HAKUNA mjamzito atakayejifungua kwa shida katika Hospitali ya Muhimbili” ni ahadi aliyoitoa Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto leo wakati akiratibu zoezi la uwekaji wa vitanda katika Wodi ya Wazazi, anaandika Hamisi Mguta.

Akizungumza katika kipindi moja kwa moja ‘live’ cha ‘Super Mix’ cha East Africa Radio amesema, kufanyika kwa zoezi hilo ni kufuatia agizo la Rais John Magufuli la kubadili matumizi ya Wizara ya Afya, Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuwa kuwa wodi ya wazazi.

Ummy amesema, Rais Magufuli anataka suluhisho la matatizo na sio michakato ya utatuzi na kwamba, atahakikisha wizara yake inakwenda sambamba na yale ambayo rais angependa kuyaona katika utawala wake wa awamu ya tano.

“Mimi ni mwanamke, na nimeshajifungua mara mbili, najua uchungu wa uzazi, sitakubali wakinamama wateseke kwa kujifungua, leo mama atalala kitandani,” amesema.

“HAKUNA mjamzito atakayejifungua kwa shida katika Hospitali ya Muhimbili” ni ahadi aliyoitoa Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto leo wakati akiratibu zoezi la uwekaji wa vitanda katika Wodi ya Wazazi, anaandika Hamisi Mguta. Akizungumza katika kipindi moja kwa moja ‘live’ cha ‘Super Mix’ cha East Africa Radio amesema, kufanyika kwa zoezi hilo ni kufuatia agizo la Rais John Magufuli la kubadili matumizi ya Wizara ya Afya, Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuwa kuwa wodi ya wazazi. Ummy amesema, Rais Magufuli anataka suluhisho la matatizo na sio michakato ya utatuzi na kwamba, atahakikisha wizara…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Hamisi Mguta

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!