Gazeti la MwanaHALISI – Taarifa kwa Umma

KATIKA toleo lake la Jumatatu, Na. 328 la Februari 29 – Machi 6, 2016 kulitokea kosa la kutokuwepo kwa habari iliyoongoza gazeti ikiwa na kichwa habari – Mkapa, Kikwete kuzuia majipu yao.

Habari hiyo, ikifuatana na picha mbili kubwa, ilianza ukurasa wa mbele na kutarajiwa kuendelea katika ukurasa wa 2. Hata hivyo, kutokana na makosa wakati wa utengenezaji kurasa, haikuwepo.

Mhariri wa MwanaHALISI anasikitika kwa kasoro hiyo ya kukosekana kwa habari hiyo, na anawaomba radhi wasomaji wote pamoja na umma kwa ujumla kwa kujikuta kwenye mtanziko baada ya kununua gazeti.

Uongozi wa gazeti la MwanaHALISI unatoa ahadi kwa umma kwamba timu ya kusimamia gazeti, itaendelea kusimamia kazi kwa umakini zaidi ili kuepuka makosa yanayoweza kuepukika.

Mhariri Mkuu

KATIKA toleo lake la Jumatatu, Na. 328 la Februari 29 – Machi 6, 2016 kulitokea kosa la kutokuwepo kwa habari iliyoongoza gazeti ikiwa na kichwa habari – Mkapa, Kikwete kuzuia majipu yao. Habari hiyo, ikifuatana na picha mbili kubwa, ilianza ukurasa wa mbele na kutarajiwa kuendelea katika ukurasa wa 2. Hata hivyo, kutokana na makosa wakati wa utengenezaji kurasa, haikuwepo. Mhariri wa MwanaHALISI anasikitika kwa kasoro hiyo ya kukosekana kwa habari hiyo, na anawaomba radhi wasomaji wote pamoja na umma kwa ujumla kwa kujikuta kwenye mtanziko baada ya kununua gazeti. Uongozi wa gazeti la MwanaHALISI unatoa ahadi kwa umma kwamba…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Masalu Erasto

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube