ANNA Gidarya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Manyara ameeleza kuwa, gari lake limeshambuliwa kwa risasi leo tarehe 16 Septemba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Anna amesema, risasi hizi zimepiga kwenye matari yake ya gari na Sasa anaelekea katika Kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kutoa maelezo.
Anaeleza kuwa, shambulizi hilo limetokea katika Kata ya Majengo, wilayani Monduli katika Mkoa wa Arusha.
Mbunge huyo anaeleza kuwa, yupo Monduli kusimamia na kufuatilia uchaguzi wa ubunge kwenye Jimbo la Monduli leo.
Leave a comment