Gambo ajitosa Ubunge Arusha Mjini, Nanai aenda Kawe

Spread the love

MRISHO Gambo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, amechukua fomu kuwania Ubunge Arusha Mjini ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea)

Gambo amechukua fomu leo Jumanne tarehe 14 Julai 2020 kuwania kupitishwa na CCM kuwania ubunge wa Arusha Mjini.

Mbunge anayemaliza muda wake wa jimbo hilo ni Gobdless Lema wa Chadema.

Soma zaidi hapa

Lema; Hata mkiniletea Ccm wote Arusha, nitashinda

Gambo alikuwa mkuu wa mkoa kwa zaidi ya miaka mitatu hadi tarehe 19 Juni 2020 Rais John Pombe Magufuli alipotengua uteuzi wake na kumteua Idd Kimanta.

Soma zaidi hapa 

Rais Magufuli ataja kilichomng’oa Gambo

Gambo alitenguliwa pamoja na viongozi wengine wakiwemo mkuu wa wilaya ya Arusha na Mkurugenzi kwa kile alichoeleza viongozi hao kutokuwa na mahusiano mazuri ya kikazi.

Wakati Gambo akijitoza Arusha Mjini, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Francis Nanai amechukua fomu kuwania Ubunge wa Kawe jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Jimbo hilo limeongozwa kwa miaka kumi mfululizo na Halima Mdee wa Chadema kuanzia 2010-2020

MCL ni wazalishaji wa magazeti ya Mwananchi, MwanaSpoti na The Citizeni.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

MRISHO Gambo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, amechukua fomu kuwania Ubunge Arusha Mjini ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea) Gambo amechukua fomu leo Jumanne tarehe 14 Julai 2020 kuwania kupitishwa na CCM kuwania ubunge wa Arusha Mjini. Mbunge anayemaliza muda wake wa jimbo hilo ni Gobdless Lema wa Chadema. Soma zaidi hapa Lema; Hata mkiniletea Ccm wote Arusha, nitashinda Gambo alikuwa mkuu wa mkoa kwa zaidi ya miaka mitatu hadi tarehe 19 Juni 2020 Rais John Pombe Magufuli alipotengua uteuzi wake na kumteua Idd Kimanta. Soma zaidi hapa  Rais Magufuli ataja kilichomng'oa Gambo Gambo alitenguliwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!