Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Fuvu la Zinjanthropus kutowekwa hadharani
Habari Mchanganyiko

Fuvu la Zinjanthropus kutowekwa hadharani

Fuvu la mtu wa kale
Spread the love

DAKTARI Hamis Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii amesitisha mpango wake wa kupeleka fuvu la mtu wa kale katika Makumbusho ya Olduvai, Ngorongoro kutokana na sababu za kisalama. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Dk. Kigwangalla ametoa kauli hiyo leo tarehe 14 Juni 2019, katika akaunti yake ya Twitter, ikiwa ni siku moja tangu Rais John Magufuli kueleza kwamba, fuvu hilo lilikuwa kwenye mpango wa kuibiwa.

Rais Magufuli wakati akizungumza na wavumbuzi wa mitambo ya umeme Ikulu, Jijini Dar es Salaam jana tarehe 13 Juni 2019 alisema “nimesikia hata fuvu la mtu wa kale lilikuwa kwenye ‘plan’ (mpango) ya kuibiwa, hii ndiyo Tanzania.”

Katika andiko lake kwenye akaunti ya Twitter, Dk. Kigwangalla amesema, alipanga kulipeleka fuvu hilo kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu kuvumbuliwa kwa fuvu la binadamu wa kale duniani la Zinjanthropus, yaliyopangwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

“Wakati nikipokea tuzo ya Hifadhi Bora Afrika iliyotolewa na World Travel Awards kwa Serengeti, nilitangaza kuwa mwaka huu tutasherehekea miaka 60 ya Zinjanthropus, na niliahidi kulipeleka fuvu halisi makumbusho ya Olduvai, Ngorongoro. Kwasababu za kiusalama hatutolipeleka! ,” ameandika Dk. Kigwangalla.

Mapema mwezi huu Dk. Kigwangalla aliwaahidi Watanzania kwamba, fuvu hilo litawekwa hadharani kwa muda wa siku tano kuanzia Julai 17 mwaka huu, na kuwataka Watanzania kutumia fursa hiyo ili kuliona fuvu hilo linalohifadhiwa katika sehemu maalum na serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!