Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Fukuto Chadema Ubungo: Katibu ‘walikiuka mwongozo’
Habari za Siasa

Fukuto Chadema Ubungo: Katibu ‘walikiuka mwongozo’

Spread the love

FUKUTO la kutimuana katika Jimbo la Ubungo, linashika kasi huku Katibu wa Kanda ya Pwani akisema, viongozi Wilaya ya Ubungo walikiuka mwongozo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kutokana na kukiukwa kwa muongozo uliotolewa na Kamati Tendaji ya Kanda, tarehe 11 Julai 2020, uongozi huo ulivunja uongozi wa majimbo ya Ilala, Temeke na Ubungo.

Taarifa zaidi zinaeleza, Kanda ya Pwani ilivunja uongozi wa majimbo hayo kwa madai ya kutosimamia vizuri utekelezwaji wa muongozo wa Chadema, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Hemed Ally ambaye Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, jana tarehe 14 Julai 2020, alisema Kamati Tendaji ya Chadema katika kanda hiyo, ilitoa muongozo wa uchaguzi kwa viongozi wa majimbo yote 19 ya kanda hiyo

Lakini viongozi wa Chadema mkoani Pwani na katika majimbo ya Ilala, Temeke na Ubungo, walikwenda kinyume na muongozo huo, hali iliyopelekea kamati hiyo kuvunja uongozi huo.

“Kwa maana ya kuweka vigezo hivyo, ilitakiwa vitekelezwe kwa sababu ni makubaliano tuliyowekeana, sio kwa Jimbo la Ubungo peke yake, ni majimbo yote 19 ya Pwani, majimbo yote walituletea kile ambacho wamekifanya kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi, Jimbo la Ubungo, Temeke, Ilala wamefanya vibaya,” amesema Hemed.

Amesema, licha ya uongozi huo kufanya vibaya, uliidanganya Kamati Tendaji ya Chadema Pwani, kwa kuipelekea ripoti ya uongozo kuhusu utekelezwaji wa muongozo huo.

Soma zaidi hapa

Kura za maoni: Chadema Ubungo kwapasuka

“Kanda ya Pwani tulienda kuhakiki kata kwa kata, Kamati Tendaji ya Kanda wakazunguka kata zote 235, tulichokwenda kukikuta ni tofauti na kilichoandikwa kwamba wamefanya.

“Tulipokaa kwenye kikao cha tahimini kwa sauti moja, tarehe 11 Julai 2020, Kamati Tendaji iliridhia kwamba maandalizi haya ya uchaguzi katika majimbo, yalikuwa mabovu na uongozi wake uvunjwe,” amesema Hemed.

Amesema, walifanya nao vikao vya tathimini, wakagundua kwenye majimbo hayo kuna shida na ndipo walipeleka ripoti katika kikao cha kamati tendaji.

“Kwa pamoja tukaridhia uongozi wa  majimbo hayo wasimamishwe, lakini sanjari na hilo, baadhi ya majimbo wapewe onyo kali kwa kutofanya vizuri,” amesema Hemed.

Alipoulizwa muongozo huo ulikuwa na masuala gani ambayo viongozi hao walishindwa kutekeleza, Hemed amesema, hawezi kutaja masuala hayo kwa kuwa ni siri za chama, hivyo maadili ya Chadema hayamruhusu.

Jana baadhi ya waliokuwa viongozi wa Chadema Jimbo la Ubungo, wakiongozwa na Renatus Pamba, aliyekuwa mwenyekiti wa jimbo hilo, kupitia mkutano wao na waandishi wa habari, walidai wamefukuzwa kwa kuwa walikuwa tishio kwa mtia nia wa kugombea Jimbo la Ubungo, ambaye anaungwa mkono na uongozi wa juu wa Chadema.

Akizungumzia kuhusu sakata hilo, Hemed amesema uongozi huo ulivunjwa ili kuepusha mipasuko kuelekea uchaguzi huo.

“Jimbo la Ubungo lipo kwenye mgogoro kwa muda mrefu. Mvutano wa kisiasa ulianza wa kawaida, lakini baadaye ulishamiri kiasi cha kudhoofisha chama. Mivutano inapotokea, uongozi wa juu unapaswa kuchukua hatua ili kukinusuru chama,” amesema Hemed.

Na kwamba, uongozi huo umevunjwa kwa mujibu wa Ibara ya 6 ya Katiba ya Chadema, inayoelekeza uongozi wa eneo fulani kuvunjwa kama utashindwa kuwajibika na kutimiza wajibu wake.

“Baada ya uongozi kuvunjwa, tulifanya ujazaji wa viongozi, na utaratibu uko wa aina mbili, wa kwanza mamlaka ya uongozi wa juu kuteua viongozi wa muda, wa pili ni uchaguzi, sisi tukaona kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi, tuweke uongozi ambao hautaletea migogoro,” amesema Hemed na kuongeza:

“Lakini tukawapa watu wa Ubungo haki ya kuchagua viongozi wao, watu wowote wanaotaka waombe, watu walijitokeza na leo wapo kwenye uchaguzi, hakuna viongozi wowote wa mwanzo walioonesha kugombea aliyekataliwa kugombea.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

error: Content is protected !!