Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Freeman Mbowe afunguka uchaguzi Kenya
Makala & UchambuziTangulizi

Freeman Mbowe afunguka uchaguzi Kenya

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

MWENYEKITI  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amefunguka na kumsifu Rais Uhuru Kenyatta kuwa mvumilivu na kuheshimu Wakenya baada ya kumalizika uchaguzi mkuu mwezi uliopita, anaandika Mwandishi wetu.

Mbowe amesema Kenyatta ameonyesha ukomavu kwa Marais wenzake wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla kwa kuwa aliruhusu kufanyika maandamano na kuamuru polisi kutoa ulinzi.

Akizungumza na kituo cha redio cha EATV leo asubuhi, Mbowe amesema Kenya wameonyesha ukomavu na vyombo vyao vya kutoa haki pia vimeonyesha kwamba vipo huru na haviingiliwi na mtu yoyote.

Amesema kitendo cha Mahakama ya Juu nchini humo kuamuru uchaguzi mkuu urudiwe hakinabudi kuigwa na nchi nyingi za Afrika.

Mbowe amesema katika kipindi chote tangu uchaguzi umalizike mwezi uliopita, Kenyatta amezidi kuonyesha ukomavu wa kisiasa na kwamba angeamua kutumia vyombo vya dola ambavyo vipo chini yake angeweza kuendelea kutawala lakini yeye hakutaka kufanya hivyo.

Mahakama ya Juu nchini Kenya jana ilifuta  ushindi wa rais Uhuru Kenyatta katika Uchaguzi uliofanyika tarehe 8 mwezi uliopita.

Uamuzi huo ulitangazwa na Jaji Mkuu David Maraga jijini Nairobi Ijumaa asubuhi. Jaji Maranga alisema kuwa kati ya Majaji sita waliosikiliza kesi hiyo, wanne walifikia uamuzi kuwa uchaguzi huo haukufanyika kwa mujibu wa Katiba ya sheria za Uchaguzi nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!