February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Fomu namba 34 A yazua utata uchaguzi Kenya

Raila Odinga

Spread the love

MUUUNGANO wa NASA, umetangaza kukataa matokeo huku ukisema matokeo yanayotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya, hayana ushahidi wa fomu namba 34 A kama sheria inavyosema, anaandika Irene Emmanuel.

NASA wameomba kukutana na Tume hiyo ili kuangalia ushahidi wa fomu hiyo ya 34 A umefuatwa.

Tamko la NASA limesema kinafanywa sasa na Tume kwa kuacha kuunganisha matokeo na fomu hiyo ambayo ilitakiwa kujazwa na Mawakala na kusainiwa nmi ukiukwaji wa sheria ya uchaguzi.

NASA amesema mpaka sasa fomu hiyo haijaonyeshwa hadharani kwa umma ama wananchi ili wajue matokeo halisi.

Odinga anasema matokeo yote yameathirika kutokana na hiyo fomu kutoonekana.

Kambi ya NASA imeeleza kuwa mengi yamekuwa yakitokea katika uchaguzi huo ikiwemo kuonekana kwa aliyekuwa mtaalamu wa IEBC, Marehemu Chris Musando akiwa bado anaingia katika akaunti ya tume.

error: Content is protected !!