Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Michezo FIFA ‘yamtupa jela’ Rais wa CAF miaka mitano
Michezo

FIFA ‘yamtupa jela’ Rais wa CAF miaka mitano

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf), Ahmad Ahmad
Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) limemfungia kujihusisha na shughuli za moita wa miguu kwa miaka mtano, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf), Ahmad Ahmad baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka sheria kadhaa za maadili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ahmad ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Fifa, amedaiwa kukiuka sheria ya maadili inayohusisha jukumu lake la utiifu, kwa kutoa na kupokea zawadi hatua ambayo ni kinyume na wadhfa wake mbali na utumizi mbaya wa fedha.

Taarifa iliyotolewa na Fifa ilieleza kuwa, uchunguzi dhidi ya Rais huyo wa Caf ulianza mwaka 2017 hadi 2019 ulihusu masuala ya utawala wake katika shirikisho hilo pamoja na kuandaa na kufadhili safari ya kuhiji Makka, kuhusishwa kwake katika kashfa ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Tactical Steel na shughuli nyengine.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa na Kamati ya Maadili ya Fifa, Ahmad ambaye anatokea nchini Madagascar alitangaza lengo lake kuwania muhula wa pili wakati uchaguzi wa Caf utakapofanyika mwezi Machi mwaka ujao.

Hilo huenda lisifanyike kwa sababu atalazimika kupita mtihani wa maadili ili kustahiki kusalia katika baraza la Fifa.

Uwezekano wa yeye kuchaguliwa kwa awamu ya pili utategemea iwapo atashinda kesi ya rufaa aliowasilisha katika mahakama ya kutatua mizozo ya michezo CAS, huku kesi hiyo akihakikisha kuwa inasikilizwa mapema ili kumruhusu kuthibitishwa kuwa mgombea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!