Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya FCS yazindua kampeni ya wanaohudumia wagonjwa wa corona
Afya

FCS yazindua kampeni ya wanaohudumia wagonjwa wa corona

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga
Spread the love

FOUNDATION for Civil Society (FCS) imezindua Kampeni ya ‘Jumanne ya Utoaji’ kuwasaidia na kuwalinda watoa huduma wa afya nchini Tanzania. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Lengo la Kampeni ya mwaka huu ni kukusanya vifaa vya kujikinga (PPE) na maambukizi ya corona (COVID-19) kwa ajili ya watoa huduma hao kama hatua ya dharura ya kuitikia mahitaji yaliyosababishwa na mlipuko wa homa hiyo ya mapafu.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga alisema kuwa kampeni hiyo inawaalika wadau na umma kwa ujumla kuchangia pesa au vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Corona kama vile barakoa, sabuni, vitakasa mikono, mavazi maalum ya watoa huduma, miwani ya upasuaji kwa ajili ya watoa huduma wa afya ambao wako mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa FCS imesukumwa kufanya hivyo kutokana na taarifa zinazotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhamasisha watoa huduma ya afya kuwa na mahitaji ya kujikinga.

“Shirika la Afya Duniani (WHO) linaripoti kuwa kila mwezi wahudumu wa afya duniani kote wanahitaji vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

“Vifaa hivi huwalinda wahudumu wa afya pamoja na wagonjwa wengine dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona, lakini kutokana na uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo duniani, watoa huduma wengi hushindwa kupata vifaa hivyo .

“Kwakuwa wahudumu wa afya wanahudumia na kuilinda jamii, wanajamii lazima waungane kwa mshikamano kuonyesha shukrani na  kuwasaidia watoa huduma hawa katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

“Kampeni hii imepewa kauli mbinu ya ‘Tujikinge, Tuwakinge Wahuduma Wa Afya’ itaendeshwa kwa wiki mbili kuanzia tarehe 21 Aprili hadi 5 Mei 2020. Kwenye kilele cha Kampeni hiyo vifaa  vitakavyopatikana vitatolewa kwa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) tarehe 5 Mei 2020.

“Kampeni hii ni harakati ya Jumanne ya Utoaji iliyozinduliwa mwaka 2012 na Umoja wa Mataifa (UN)  na Shirika la 92Y huko New York Marekani, kwa lengo la kusherehekea uhisani, na utoaji kwa kuchangia kuwasaidia wenye uhitaji.

“Kampeni hii ya Jumanne ya Utoaji imekuwa ikiandaliwa na kufanyika kila mwaka na kusherehekewa ulimwenguni kote. Nchi nyingi, makampuni, wafanyabiashara, shule, watu binafsi, familia na AZAKi husherekea kampeni hii.

“FCS imekuwa ikiendesha Kampeni hii ya Jumanne ya utoaji nchini kwa miaka 4 sasa kama njia ya kukuza moyo wa kusaidia wenye uhitaji,Mwaka jana, Kampeni hiyo ililenga kuwasaidia watoto wenye ulemavu wapatao 228 wanaosoma Shule ya Msingi ya Matumaini jijini Dar es salaam. Thamani ya vitu vyote vilivyotolewa kwa wa walezi wa watoto hao siku hiyo ilikuwa zaidi ya Sh milioni 9.5,” alisema Kiwanga.

Kiwanga ameongeza kwa kusema kuwa, watoa huduma wa afya wanawahudumia watu wanaoshukiwa au wagonjwa waliothibitika kuambukizwa COVID-19. Ni muda muafaka sasa kama jamii kuungana na kuonyesha shukrani kwa watoa huduma ya afya.

Alisemakuwa hivi karibuni FCS kwa kuongeza juhudi za kuchangia fedha kwenye Mpangokazi wa kitaifa wa kupambana na Virusi vya Corona, AZAKi 10 zilichangia kiasi cha shilling Tsh Milioni 79 Serikalini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!