Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Fatma Karume: Siku ya kufa ni moja, sitishwi
Habari za SiasaTangulizi

Fatma Karume: Siku ya kufa ni moja, sitishwi

Spread the love

MWANAHARAKATI na mkosoaji mkubwa wa serikali ya awamu ya tano, Fatma Karume amesema, vitendo vya utekaji wanavyofanywa dhidi ya wanaharakati wengine, havimtishi wala kumjengea hofu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, kila aliyeumbwa na Mungu anayo siku yake moja ya kufa, na kwamba watesaji wanaolipwa kwa sababu hiyo ama kuua, nao siku yao ya kufa itafika – watakufa.

Fatma ambaye ni Rais Mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na mtoto wa Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Mapinduzi (Zanzibar), Amani Abeid Karume, ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Januari 2020.

Ametoa kauli hiyo baada ya kuulizwa na mwandishi wa MwanaHALISI Online, kwamba vitendo vya utekaji vinavyokomaa nchini, havimtishi kwenye harakati zake?

“Binadamu ukishazaliwa, ujue itafika siku yako ya kufa sababu ni wajibu kufa, siku moja nitakufa, na siwezi kumzuia Israel kuja na ataletwa kwa namna yake,”amesema na kuongeza “siku ya kufa ikija, mimi nitakuwa nimekufa, wao (watekaji, wauaji) watabaki,” ameeleza Fatma.

Fatma amesema, anachojua ni kuwa hakuna atakayesalia kwenye ulimwengu huu, na kwamba wanaoua na wanaotuma kuua nao watakufa, kwa kuwa kifo ni haki ya kila mmoja.

“Hata kama watu wasiojulikana watabeba dhamira ya kuniua, nitakufa tu, na hata wasiponitafuta kuniua, nitakufa tu, kwa kuwa kifo ni haki yangu, sina sababu ya kuhofia hilo,” aemesema.

Kwa mujibu wa mwanaharakati huyo, ukiukaji wa haki za binadamu nchini, umekomaa kulinganisha na awamu zilizopita.

“Ukiukwaji wa haki za binadamu ulikuwepo tangu zamani, sheria za vizuizi chini ya Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa ukiukwaji wa haki binadamu.

“Chini ya babu yangu kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu. Wao walikuwa wanajitetea kwa kusema nchi changa, mimi siamini kwa nchi changa sababu misingi lazima iwe ya haki. Uchanga wa nchi sio sababu ya kukiuka haki za binadamu,” amesema Fatma.

Mjukuu huyo wa muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya 12 Januari 1964 na Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Abeid Amani Karume amesema, haki za binadamu lazima ziwe msingi wa nchi, “ukianza kukiuka haki, kurudi ni vigumu.”

Fatma amesema, hawezi kuvumilia kuona misingi ya haki za binadanu inakiukwa, na kwamba ataendelea kutumia taaluma yake ya sheria kupinga ukiukwaji wa haki hizo.

“Siwezi kustahilmili huu uonevu, kutokufuata taratibu za sheria. Siwezi kuvumilia huu ujinga sababu hatukupata Uhuru ili kukandamizana namna hii,” amesema Fatma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!