January 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Epl yalejea Arsenal, Liverpool, Man City vitani

Spread the love

BAADA ya kupoteza kwa mchezo kwa mabao 7-2 klabu ya Liverpool kesho watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Goodson Park kujiuliza dhidi ya majirani zao Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England utakaochezwa majira ya 8 mchana. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ligi hiyo ambayo ilisimama kwa wiki moja kupisha michezo ya kimashindano na kirafiki ya kimataifa iliyopo kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) na kesho itashuhudiwa michezo 10 kupigwa kwenye viwanja tofauti.

Katika mchezo huo Liverpool itapata huduma ya wachezaji wao Thiago Alcantara na Sadio Mane ambao walikosekana kwenye mchezo uliopita kutokana kuwa na majeruhi.

Michezo mingine kwenye ligi hiyo itashuhudia Arsenal wataivaa Manchester City kwenye Uwanja wa Etihad, Newcastle United wataialika Manchester United, Chelsea dhidi ya Southampton, Sheffield United kuikabili Fulham na Tottenham dhidi ya West Ham United.

Mpaka sasa Everton wapo juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 12 wakifuatiwa na Astorn Villa kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 9 sawa na Leicester City, Arsenal na Liverpool.

error: Content is protected !!