Elisha wa TBC aagwa Dar, kuzikwa kesho  

Spread the love

MWILI wa Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Elisha Elia (39), umeangwa jijini Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda Tukuyu Mbeya kwa maziko kesho Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Elisha alifikwa na mauti Jumamosi iliyopita tarehe 24 Oktoba 2020 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akisumbuliwa na vidonda vya tumbo vilivyoanza kumsumbua mapema mwezi huu.

Mamia ya ndugu, jamaa na marafiki wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge wameshiriki kuaga mwili wa Elisha leo Jumatatu tarehe 26 Oktoba 2020 katika Kanisa la KKKT Usharika wa Segerea.

Akitoa salamu za Serikali, Kunenge amesema, Elisha amekuwa chuo kwa yale yote aliyoyafanya kwa taifa lale.

Elisha ameacha mjane na watoto wawili.

MWILI wa Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Elisha Elia (39), umeangwa jijini Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda Tukuyu Mbeya kwa maziko kesho Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).  Elisha alifikwa na mauti Jumamosi iliyopita tarehe 24 Oktoba 2020 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akisumbuliwa na vidonda vya tumbo vilivyoanza kumsumbua mapema mwezi huu. Mamia ya ndugu, jamaa na marafiki wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge wameshiriki kuaga mwili wa Elisha leo Jumatatu tarehe 26 Oktoba 2020 katika Kanisa la KKKT Usharika…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!