Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Elimu mpya: Je, Covid-19 vinaishi muda gani katika vitu kabla kuambukiza?
Afya

Elimu mpya: Je, Covid-19 vinaishi muda gani katika vitu kabla kuambukiza?

Spread the love

JINSI hofu ya kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19 inavyozidi kupanda, ndivyo hofu ya kushika vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuwa na virusi pia inapanda. Unaripoti Mtandao wa Shiriki la Habari la Uingereza (BBC).

Kuna baadhi ya matukio ambayo yanafanana katika maeneo ya umma duniani – watu wengine wanajaribu kufungua milango kwa kutumia viwiko, ikiwa ni namna ya kujizuia kushika vitasa vya milango ya umma.

Katika maeneo ambayo ugonjwa wa corona umeathiri kwa kiwango kikubwa, kila kona kuna makundi la wafanyakazi wa usafi wakiwa wamevaa nguo za kujikinga maambukizi wakisafisha maeneo ya wazi, hospitali, migahawa na maeneo ya maduka makubwa.

Mtu akikohoa mara moja tu, anaweza kusambaza vijidudu 3,000

Katika baadhi ya miji, watu wanaojitolea wamekuwa wakijitokeza kusafisha mashine za benki.

Kama ilivyo katika maambukizi ya kupumua mengi, mafua yakiwemo, maambukizi ya corona yanaweza kusambaa pale ambapo mtu akikohoa na vijidudu vikabaki kwenye mkono na akashika kwenye pua na mdomo.

Mtu akikohoa mara moja, anaweza kusababisha matone ya vijidudu vipatavyo 3,000.

Ukraine ina idadi ndogo ya maambukizi mpaka sasa lakini, idadi inaonekana kuongezeka.

Vijidudu vinaweza kutoka kwa mtu mmoja na kuenea kwa watu wengine, kubaki kwenye nguo na vitu vinavyowazunguka na baadhi ya vijidudu vidogo vinaweza kubaki hewani.

Kuna ushahidi wa kuwa, virusi vinaweza kuishi kwa muda mrefu zaidi kwenye kinyesi, hivyo mtu ambaye hataosha mikono yake vizuri anaweza kusambaza virusi kwenye kila kitu atakachokishika.

Ni vyema kuzingatia hayo kwa mujibu wa Kituo cha Kukabiliana na Magonjwa nchini Marekani (SDC), ambapo wanasema kuwa ukishika kitu ambacho kina virusi na ukajigusa katika uso wako, kwa kiwango kikubwa unaweza kupata maambukizi ya virusi vya corona.

Kuosha Mikono

Hata kituo cha kukabiliana na magonjwa- CDC, Shirika la Afya Duniani (WHO) na mamlaka nyingine za afya, wamesisitiza watu kuosha mikono kila mara na kuepuka kujigusagusa usoni ili kuzuia maambukizi mapya ya corona.

Ingawa bado haijafahamika ni visa vingapi vimesabaishwa kwa kushika vitu moja kwa moja, wataalamu wa afya wameshauri watu kuchukua tahadhari.

Jambo moja ambalo bado halijawekwa wazi ni muda gani virusi vya SARS-CoV-2, jina la virusi ambavyo vilisababisha Covid-19 vinaweza kukaa katika mwili wa binadamu.

Baadhi ya tafiti zinasema, kuwa virusi vingine vya corona vikiwemo vya Sars na Mers, vinaweza kukaa kwenye vitu vya chuma, glasi na plastiki kwa muda wa siku tisa, ikiwa sehemu hizo hazijafanyiwa usafi stahiki.

Huku vingine vinaweza kukaa mpaka siku 28 katika mazingira ya joto la chini.

Virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, vinadhaniwa kukaa kwa muda mrefu hewani zaidi ya kwenye vitu kama viti.

Saa kadhaa hewani

Kikohozi cha kawaida ambacho hakina maambukizi, kina udogo wa mara 30 wa nywele ya binadamu- kinauwezo wa kubaki hewani kwa saa kadhaa.

Hii ikimaanisha kuwa, virusi vinaweza kuishi katika mfumo wa dunia kwa saa kadhaa mara tu mara baada ya vijidudu hivyo vinaposambaa.

Lakini utafiti umebaini kuwa, virusi vya SARS-CoV-2 vinaweza kukaa saa 24 – na vinaweza kukaa siku 2-3 katika vitu kama plastiki au chuma.

Matokeo ya utafiti ambayo yanaeleza kuwa virusi vinaweza kukaa kwenye vitasa katika milango kwa muda mrefu.

Utafiti umebaini nini , kuwa vitu vya madini ya kopa yanaweza kuua vijidudu kwa muda wa saa nne.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya afya ya kitaifa ya Marekani (NHI), kuhusu muda gani virusi hivi vinaweza kuishi, imechapishwa katika jarida la ‘New England Journal of Medicine’ unaonyesha kuwa vijidudu hivyo vinaweza kukaa kwa muda wa saa tatu hewani baada ya mtu kukohoa.

Tunawezaje kujikinga

Lakini kuna uamuzi wa haraka, utafiti unaonesha kuwa virusi vya corona vinaweza kukingwa katika vitu kwa dawa yenye kiasi cha pombe cha asilimia 62-71, au asilimia 0.5 ya usafi wa nyumba na vitu.

Joto la juu na kinga ya mwilini ya mtu ndio husababisha virusi vya corona kufa kwa haraka, ingawa utafiti unahusisha virusi vya corona ambavyo vilisababisha Sars vinaweza kuuliwa katika hali yanyuzi joto 56°C au 132°F kati ya vidudu 10,000 kila baada ya dakika 15.

Ingawa hakuna takwimu zinazosema kama mtu mwenye maambukizi akikohoa mara moja, vijidudu vinaweza kuwa kiasi gani, utafiti wa virusi vya mafua vinaweza kupata maelfu ya vijidudu vyenye maambukizi.

Hata hivyo, hali hii inategemea na aina ya virusi vyenyewe vilivyopatikana, viko kwenye hatua gani?

Katika upande wa nguo haijafahamika vijidudu vinaweza kukaa kwa muda gani?

Kiwango cha joto

Mabadiliko ya kiwango cha joto na mazingira kinaweza kuathiri muda ambao vijidudu vinaweza kuishi katika mazingira ya binadamu.

Utafiti bado unaendelea kufanyika ili kubaini athari zinazopatikana katika hali ya kiwango cha joto na mazingira husika.

Umuhimu wa usafi wa mikono na vitu, na namna ambavyo virusi vinatoka sehemu moja kwenda kwa mwingine

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!