May 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ebola: Tanzania yaishangaa WHO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imeeleza kushangazwa na kauli ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba ilikugoma kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola. Anaripoti Faki Sosi … (Endelea).

“Sisi wenyewe tumeshangaa kwanini WHO (Shirika la Afya Duniani) wametoa taarifa ya kwamba hatujawapa sampuli? Sisi tunashangaa kwanini wametoa hiyo taarifa lakini nyie wenye ni mashahidi, mwakilishi wa WHO alisema kwamba hakuna Ebola Tanzania,” amesema Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya leo tarehe 3 Oktoba 2019.

Amesema, Tanzania hakuna ugonjwa wa Ebola na kwamba hakuna mtu yeyote aliyebainika kuwa na ugonjwa huo.

Waziri Ummy amesema, kwa sasa ugonjwa huo upo Kaskazini  mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Na kwamba, kwa kuwa DRC ipo jirani na Tanzania, serikali imeanza kuchukua za tahadhari huku akisisitiza, taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kuhusu uwepo wa ugonjwa huo nchini, hazina ukweli wowote.

“Kipaumbele chetu sisi baadala ya tuhuma na kutoaminiana kwamba tunaficha taarifa, tumeweka wataalamu kwenye mipaka,” amesema na kwamba, mipaka yote iliyokuwa rasmi na ile ambayo sio rasmi, imedhibitiwa.

error: Content is protected !!