July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dortmund, Bayern vitan leo Bundesliga

Spread the love

LIGI Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ kuendelea tena leo ambapo Borrusia Dortmund itawakaribisha klabu ya FC Bayern Munichen kwenye dimba la Signal Iduna Park katika kusaka alama tatu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo ambao unavutia wapenzi wengi wa mpira wa miguu ulimwenguni kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote mbili kwa sasa licha ya kutochezwa bila mashabiki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19.

Macho ya wengi katika mchezo wa leo yatakuwa kwa mshambuliaji kinda wa klabu ya Dortmund, Erling Haland (19) ambaye mpaka sasa ameshafunga mabao 13 toka alipojiunga na kikosi hicho kwenye dirisha dogo la usajiri akitokea klabu ya Red Bull Salzburg.

Mpaka sasa timu hizo zimekutana mara 103, Bayern imefanikiwa kushinda mara 48, huku Dortmund 26 na kwenda sare mara 26.

error: Content is protected !!