Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dodoma wajiandaa kumpokea Rais Magufuli kwa mabango
Habari Mchanganyiko

Dodoma wajiandaa kumpokea Rais Magufuli kwa mabango

Rais John Magufuli
Spread the love

WAKAZI wa Kata ya Mtumba, jijini Dodoma wanajiandaa kumpokea Rais John Mgufuli kwa mabango yenye malalamiko baada ya halmashauri ya jiji hilo kushindwa kulipa fidia zao za viwanja. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wameeleza kuwa, watafanya hivyo pale Rais Magufuli atakapokwenda kuzindua majengo ya mji wa kiserikali yaliyopo Kata ya Mtumba.

Wakizungumza na vyombo vya habari kwa wakati tofauti wananchi hao wameeleza kuwa, Halmashauri ya Jiji iliwataka kupisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa mji wa kiserikali huku wakiahidiwa kulipwa fidia ya Sh. 1.5 milioni kwa heka jambo ambalo halijatelezwa mpaka sasa.

Neema Kalumuna, mkazi wa Mtumba, Dodoma amesema kuwa Halmashauri ya Jiji imeshindwa kuwalipa fidia ambapo hata maeneo ya kulima kwa sasa yamekuwa shida.

“Tumecheleweshewa kulipa fidia na sasa ni mwaka mmoja lakini hakuna chochote. Kutokana na hilo, tunamwomba rais wetu ambaye ni mtetezi wa wanyonge atuone ili tuweze kulipwa haki zetu.

“Mama yangu amekufa bila hata kupata fidia, nimemuuguza kwa shida sana kila siku uongozi wa jiji unadai kuwa, watatulipa fidia lakini hatuoni. Mbaya zaidi fedha ambayo wanatakiwa kutulipa ni ndogo sana na hiyo wanaichelewesha, sisi tutaenda wapi,” amesema Neema.

Godwin Kunambi, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma alipotafutwa na kuzungumzia madai ya wananchi hao, alisema yupo kwenye kikao.

Erasto Mgusi, Mwenyekiti wa CCM, Tawi la Mtumba amesema kuwa, kinachofanywa na uongozi wa jiji kutowalipa wananchi fidia ni dalili za kutaka kuihujumu serikali ambayo inaongozwa na CCM kwa kuwa, wananchi wamekuwa na hasira na serikali yao.

Amesema, wananchi wamekuwa wakilalamika kwa kutolipwa fedha zao za fidia jambo ambalo linaonekana kuwa mwiba mkubwa zaidi kwao.

Mgusi amemwomba Rais Magufuli kuingilia kati mgogoro huo ili wananchi waendelee na shughuli zao na kwamba, kinachofanywa na uongozi wa jiji ni dalili mbaya za kutaka kuwagombanisha wananchi na serikali.

Faith Silla, Mwenyekiti wa Mtaa Mtumba amesema, wananchi wamekuwa wakiitukana serikali kwa madai kuwa, haiwajali watu wa hali ya chini kutokana na kinachofanywa na Mamlaka ya Halmashauri ya Jiji ya kutolipa fidia wananchi hao.

Kiongozi huo wa mtaa amesema, wananchi kwa sasa wanaonekana kupoteza matumaini na serikali huku wananchi wenye maeneo yao wakujipanga kumpokea Rais Magufuli kwa mabango yenye malalamiko.

“Huku ni mji wa kiserikali lakini pia tupo karibu na Ikulu hivyo siyo picha nzuri kuwa na malumbano kati ya wananchi na viongozi wa serikali. Ombi langu kubwa kwa Rais aingilie kati mgogoro huo ili amani iendelee kuwepo,” amesema Silla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!